Mvumbuzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uber Kajiuzulu

Baada ya kashfa za muda mrefu kwa kampuni ya Uber hatimaye imekua hivi
Travis_Kalanick Uber Travis_Kalanick Uber
Picha na Heisenberg Media

Baada ya matatizo ya hapa na pale pamoja na mashtaka yanayotokana na unyanyasaji wa kijinsia kwa wafanya kazi wake hatimaye mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Uber Travis Kalanick siku ya leo ameamua kujiuzulu rasmi, imeripoti tovuti ya The New York Times.

Kati hali hiyo ambayo ilitaraijiwa na wengi, mvumbuzi huyo wa kampuni ya uber atapoteza nafasi ya kuwa kiongozi wa kampuni hiyo lakini bado atakuwa kati ya watu watano wenye hisa kwenye kampuni hiyo. Hata hivyo hatua hii imefikiwa baada ya viongozi wengine wa juu wenye hisa kwenye kampuni ya Uber kulazimisha Travis kuachia ngazi kama kiongozi na Mtawala wa kampuni ya Uber.

Kampuni ya uber pamoja na kiongozi huyo kwa ujumla amekuwa akikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na sakata la mfanyakazi wa kampuni hiyo kunyanyaswa kijinsia, ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa juu kuacha kazi kwenye kampuni hiyo kutokana na sababu mbalimbali za unyanyasaji kazini, lakini kama haitoshi kampuni hiyo ya Uber siku za karibuni ilifukuza watu karibia 20 kutokana na uchunguzi ulio kuwa unafanyika kutokana na kile kilichosemekana kwa baadhi ya wafanyakazi hao kujihusisha na sexism au Ngono kazini.

Advertisement

Bado haijajulikana nani atakaye chukua nafasi ya kiongozi huyo lakini kwa habari zilizopo kwenye mtandao viongozi hao wa uber tayari wamesha mchagua mtu wa kuchukua nafasi hiyo lakini bado haija mtangaza rasmi kwa wafanyakazi na watumia wa huduma za Uber duniani kote.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use