Kampuni ya Uber Yakabiliwa na Kashfa ya Unyanyasaji wa Kijinsia

Uber kukabiliwa na madai ya unyanyasaji wa kijisia kwa wafanyakazi wake
KAMPUNI YA UBER KAMPUNI YA UBER

Uber ni kampuni ya usafirishaji ambayo inatumia teknolojia ya kisasa kurahisha usafiri miongoni mwa wakazi wa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania. Hivi karibuni kampuni hiyo ilikubwa na kashfa nzito kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko San Francisco nchini Marekani.

Katika kashfa hiyo mfanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo Susan Fowler Rigetti, aliandika kwenye makala ya blog yake ya Susan J. Fowler, kuwa katika kipindi alichokua anafanya kazi kwenye kampuni hiyo kama Engineer yeye pamoja na wafanyakazi wengine wa kike walikutana na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ubaguzi kutoka kwenye menejimenti ya rasilimali watu (Human Resources) ya kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya the washington post, mara baada ya Susan kuanza kazi kwenye kampuni ya uber alipokea ujumbe mfupi kutoka kwa meneja wake akiwa anataka kuanzisha mahusiano na yeye. Tovuti hiyo iliendelea kuandika kuwa mfanyakazi huyo alichukua hatua ya kwenda kushtaki kwenye menejmenti ya rasilimali watu na alijibiwa kuwa hilo lilikuwa ni kosa la kwanza kwa meneja huyo hivyo hawana budi kumsamehe na susan alishauriwa kuhamia kwenda kwenye timu nyingine kwenye kampuni hiyo. Baadae susan alikuja kugundua kuwa kulikua na wafanyakazi wengine wa kike ambao walikua wakitoa lawama kama hizo kwenye menejimenti ya rasilimali watu ya kampuni hiyo ya Uber kuhusu tabia ya meneja huyo.

Advertisement

Hata hivyo kampuni ya Uber imeamua kumuajiri Eric Holder ambaye alikua mwanasheria mkuu wa marekani ili kuchunguza madai hayo kwa kusaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni pamoja na viongozi wakuu Liane Hornsey pamoja Angela Padill wote kutoka kwenye kampuni hiyo ya Uber.

Kujua zaidi kuhusu sakata hili litakavyokuwa baada ya kuchunguzwa na mwanasheria huyo endelea kutembelea Tanzania Tech kilasiku au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupokea habari kwa haraka pale tu zitako toka, pia kama unataka habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use