Mtandao wa TikTok ni moja ya mtandao ambao hivi sasa unatumiwa kna watu wengi zaidi hasa hapa Tanzania. Kutokana na hio watu wengi zaidi wamekuwa wakitumia mtandao huo kuweka video mbalimbali ambazo zimeonekana kufurahisha watu.
Sasa kama ulikuwa hujui Instagram na mitandao mingine ya kijamii haipendi video zinazowekwa ambazo zina alama ya Tik tok, hii hufanya video hizo kuto wafikia watu wengi zaidi.
Lakini kwa kutumia njia hii utaweza kuondoa alama iliyopo kwenye video yoyote ya TikTok na kuweza kutumia kwenye mitandao mingine kama Instagram, YouTube na hata Facebook.
Wakati tukiwa bado tuna andaa makala ya jinsi ya kutumia njia hii kwa watumiaji wa iOS au iPhone, hebu leo tuanze na watumiaji wa Android.
Kupitia njia hii unaweza kutumia kupakua video zote zilizopo kwenye mtandao wa TikTok bila video hizo kuwa na alama ya username ya mwenye video pamoja na logo yake.
Kama unataka kuona jinsi njia hii inavyofanya kazi unaweza kubofya Play hapo chini, au unaweza kuendelea kwa kupakua app hapo chini ya video. Kumbuka app hii hapatikani Play Store.
Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, video hiyo baada ya kudownload haina alama kwenye kona yenye logo ya TikTok pamoja na username.
Kupitia njia hii utaweza kupakua picha iliyoko kwenye video pamoja na muziki pekee ambao umetumika kwenye video husika.
Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube kwani tumeanzisha kipengele kipya cha maujanja dakika ambapo utaweza kujifunza kwa haraka zaidi. Hakikisha una subscribe kuanza kujifunza leo.
habari za asubuhi naomba kuuliza hivi Airtel master card au m pesa master card zinauwezo wa kupokea pesa mtandaoni kama vile amazon paypal na google play store?
Kwa sasa sijajua kama zinao uwezo huo