Ukweli ni kwamba kila mtu anapenda kuangalia video mpya, lakini kuna baadhi ya watu ambao wanapenda video zaidi kiasi cha kutaka kubaki na video nayo kwenye vifaa vyao. Kama wewe ni mmoja wa watu hawo basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha apps nzuri za Android ambazo unaweza kutumia ku-download video mpya kutoka kwenye mtandao wowote. Kumbuka app hizi ni maalum kwa watumiaji wa Android hivyo kama wewe unatumia simu za iPhone itakubidi kusubiri kidogo wakati tukifanya uchaguzi yakinifu jinsi ya kupata app zenye uwezo kama huu.
Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tukangalia app hizi nzuri za kusaidia kupakua video mpya kupitia simu yako ya mkononi ya Android.
SnapTube VIP
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kudownload video mpya kutoka kwenye mitandao yote ya kijamii ikiwa pamoja na kudownload nyimbo mpya kutoka YouTube basi app hii ya snaptube vip ni app nzuri sana kwako. App hii haipatikani Play Store na mara nyingi inakuwa na matangazo mengi sana lakini tumefanikiwa kuondoa matangazo kwako ili ufurahie ku download na kuangalia video mpya bila kusumbuliwa na matangazo.
Videoder
Videoder ni app nyingine nzuri sana ya kudownload video mpya kupitia simu yako ya mkononi, app hii ni nzuri sana na kama ilivyo Snaptube hii pia ina uwezo wa kupakua video kutoka mitandao yote unayo ifahamu. App hii pia inakuja na matangazo mengi sana na haipatikani kupitia soko la Play Store, lakini pia tumejitahidi kuondoa matangazo kwenye app hii hivyo sasa unaweza kufurahia video mpya bila matangazo yoyote.
NewPipe
Newpipe ni app nyingine nzuri sana kwa wapenzi wa video mpya, tofauti zilivyo app nyingine kwenye list hii, app ya NewPipe itakusaidia kupata video kupitia mtandao wa Youtube Pekee, mbali na hayo app hii ni nzuri sana kwa kupakua video na inauwezo wa kupakua video kwa haraka sana na kwa urahisi. App hii pia haipatikani kupitia soko la Play Store hivyo ni muhimu kudownload kupitia link hapo chini.
Na hizo ni ndio app nzuri ambazo unaweza kutumia kupakua video mpya kupitia simu yako ya mkononi ya Android. Kumbuka app hizi zote hazipatikani kupitia soko la Play Store hivyo ni muhimu kupakua kupitia link hapo chini. Kama wewe ni mpenzi wa nyimbo mpya unaweza kupata nyimbo zote mpya za bongo kupitia simu yako ya mkononi kwa kupakua app moja tu ya Nyubeat, unaweza kupata app hiyo kupitia link hapo chini.
Kama unataka kujua jinsi ya kudownload nyimbo mpya kupitia mtandao basi unaweza kusoma makala hii hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia na maujanja hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
nimependa sana
tunaotumia simu za batani mtandao mtandao mbn unatuxumbua xn jaman hasa ule mda ukitaka kudownload video flan n.k.