in

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Tumia njia hii kupata jina lako la biashara kwa urahisi na haraka sana

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotaka kufungua biashara yako kwa mara ya kwanza basi ni wazi kuwa jina ni kitu cha msingi sana cha kwanza kufikiria. Na kwa sababu wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi leo nimekuletea njia rahisi sana ya kupata jina lako la biashara pamoja na akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kumbuka ni muhimu sana kuchagua jina la biashara lenye kufanana na aina ya biashara yako, na pia ni vizuri zaidi kama jina lako litakuwa na maana kwa namna moja ama nyingine au lenye mwitikio mzuri wa ladha pale linapo tamkwa.

Pia kumbuka ni muhimu kuchagua jina ambalo halipo hasa mtandaoni kwani hii itasaidia sana biashara yako kusimama pekee pale mtu anapo tafuta jina la biashara yako kupitia mtandao. Pia usisahau kutafuta domain yenye jina lako ya .COM kwani hii ni muhimu sana kwenye kila biashara iliyopo mtandoni siku hizi, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata domain kwa Tsh 3,000 tu.

Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twenda tuangalie njia hii rahisi ya kupata jina la biashara pamoja na akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kwa kuanza zipo tovuti nyingi sana ambazo zinaweza kukusaidia kufanya hivi, kupitia hapa nitaweza kuonyesha baadhi tu ya tovuti ambazo ni bora sana kwenye kutafuta majina ya biashara pamoja na majina ya akaunti za mitandao ya kijamii.

Habari Kubwa za Teknolojia Wiki Hii Tarehe 29/08/2020

YALIYOMO

Namechk

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Namechk ni tovuti nzuri sana ambayo itakusaidia kutafuta jina lako la biashara, tovuti pamoja na akaunti zako za mitandao ya kijamii, tovuti hii ni rahisi sana kutumia na utaweza kupata jina lako kwa haraka sana. Unachotakiwa kufanya ni kuweka jina lako kwenye sehemu ya kutafuta na baada ya hapo tovuti hii itakuletea majibu kama jina hilo limesha chukuliwa ikiwa pamoja na mitandao ya kijamiii.

TEMBELEA NAMECHK HAPA

Namecheckr

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Namecheckr ni tovuti nyingine ambayo inaweza kukusaidia sana kupata akaunti zako za mitandao ya kijamii. Tofauti na tovuti iliyopita, tovuti hii inaweza kusaidia kupata username ya akaunti yako kwa urahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kuweka jina ambalo unahitaji kwenye sehemu ya kutafuta na pale unapo ona alama ya tiki kwa pembeni kwenye logo ya mtandao husika basi hapo maana yake ni kuwa jina hilo linapatikana.

TEMBELEA NAMECHECKR HAPA

Namelix

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Namelix ni tovuti nyingine nzuri sana ambayo itakusaidia kupata jina la biashara, tovuti hii ni nzuri sana kwa sababu inatumia mfumo wa AI kuweza kutengeneza jina la biashara ambalo linaweza kuendana na matumizi yako. Tofauti na tovuti zote zilizopita, tovuti hii itakusaidia kutengeneza jina la biashara kutokana na herufi au maneno fulani, kwa mfano unaweza kuandika teknolojia au neno lolote na tovuti hii itakusaidia kutengeneza logo na jina zuri ambalo unaweza kutumia kwenye biashara yako.

Game ya PUBG na App Nyingine 117 Zazuiwa Nchini India

TEMBELEA NAMELIX HAPA

Business Name Generator

Kupata Kwa Haraka Jina la Biashara na Akaunti za Mitandao ya Kijamii

Tovuti nyingine ambayo inaweza kukusaidia kupata jina la biashara kwa urahisi ni tovuti ya Business Name Generator, tovuti hii kama tovuti iliyopita itaweza kukusaidia kupata jina la biashara kwa kuandika herufi au neno ambalo linafanana na jina la biashara yako na baada ya hapo tovuti hii itaweza kuletea jina ambalo linaweza kufaa kwenye biashara yako.

TEMBELEA TOVUTI HII HAPA

Na hizo tu ndio baadhi ya tovuti ambazo zinaweza kusaidia kurahisisha kazi ya kutafuta jina bora la biashara, kumbuka mara baada ya kupata jina lako la biashara ni wakati sasa wa kusajili jina la biashara yako kupitia BRELA na kutokana na taarifa mpya za BRELA sasa unaweza kusajili kampuni nzima kupitia mtandao, unaweza kuanza kusajili biashara yako kupitia mtandao wa BRELA HAPA.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.