in

Jinsi ya Kununua Domain ya .COM kwa Shilingi Tsh 3,000

Jinsi ya kupata domain kwaajili ya tovuti yako kwa gharama nafuu

Jinsi ya Kununua Domain ya .COM kwa Shilingi Tsh 3,000

Linapokuja swala zima la biashara ni wazi kuwa huwezi kufanya biashara kikamilifu bila kuwa na tovuti, tovuti imekuwa ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mfanya biashara na wateja hivyo nadhani ni muhimu sana kwa kila biashara kuwa na tovuti.

Kuliona hili hivi leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia ili kuweza kuanzisha tovuti yako kwa gharama nafuu, njia hii ni nzuri sana na endapo ikichanywa na njia nyingine za kutengeneza tovuti bila kutumia gharama yoyote ambazo tayari tulisha ziangalia hapo awali.

Basi hebu tuache maneno mengi na twende kwenye njia hii, sasa kama kichwa cha makala kinavyosema hapa tutaenda kuangalia njia ya kupata domain yenye .com ambayo ndio itakusaidia kutengeneza tovuti kwa gharama ya Tsh 3000 pekee. Kumbuka njia hii ni bora kama unataka kufuta njia za kutengeneza tovuti ya bure ambazo zimewahi kuonyeshwa kwenye makala zilizopita.

Sasa kwa kuanza unatakiwa kubofya Link HAPA kisha utapelekwa kwenye ukurasa wa tovuti ya GoDaddy ambayo ni tovuti maarufu sana kwa usajili wa domain. Kwenye ukurasa huu unatakiwa kuchagua domain ya .COM kwa gharama za hadi dollar $0.99.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Jinsi ya Kununua Domain ya .COM kwa Shilingi Tsh 3,000

Najua utakuwa unajiuliza kwanini ni dollar 0.99 ambayo ni Tsh 2,000 na mimi nina kwambia Tsh 3,000, sasa uatakapo fika kwenye sehemu ya malipo utaona gharama zimeongezeka hadi kufikia dollar $1.17 ambayo ni takribani Tsh 2700.

Lakini sasa kama huna kadi ya benki kuweza kulipia domain hii unaweza kulipia kwa kutumia Mpesa, unacho takiwa ni kufuata maelezo ya jinsi ya kutengeneza Mpesa Mastercard na baada ya kumaliza weka namba za kadi utakazo kuwa umetumiwa kwa njia ya SMS bila kusahau mwezi na mwaka wa kadi yako kuisha pamoja na CVC.

Baada ya hapo lipia na moja kwa moja utakuwa umemaliza na utapata domain yako kwa kiasi cha Tsh 3,000 tu. Kumbuka unaweza kufuata hatua hapo chini ili kuweza kuunganisha website yako pamoja na domain yako.

Na hiyo ndio njia rahisi sana ya kupata domain ya .COM kwa Tsh 3,000. Kama kuna mahali umekwama usiache kutuambia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tuta kusaidia moja kwa moja.

Jackline John

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Maoni 13

Toa Maoni Hapa
  1. Nataka Kujua Jinsi Ya Kutoa Logo Ya RenderForest Pindi Ninapodownload Au Ninapotengeneza Logo I Mean Video Intro Au Kuhusu Upande Wa Malipo Inakuwaje

  2. Kweny hizo ip adress zote zmekataaa hapo ndo nimeishia inasema cname must have a name japokuwa nmeweka A na sio CNAME

  3. asante sana kwa kutupa maujanja na je vipi gharama za kuihost hiyo tovuti ni zachini pia kama ilivyo domen yake?

  4. Mimi blog yangu ni Wakwetusote.blogspot.com na domain ni Zantech.tk niliitengeza kupitia freenom sasa haijawa kikwazo cha kuto approved AdSense?maana hio domain ni free

  5. Mimi nimejaribu kusajiri domain zayumba.com godady Ila inakataa ikifika sehemu y malipo nakutumia M-Pesa MasterCard. Naomba mnisaidie hapo inakuje? Angela nimeweka kabisa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.