Google Yanunua Sehemu ya Timu ya HTC kwa Dollar Billion $1.1

Google yanunua wataalamu 2,000 kutoka kampuni ya HTC
Kampuni ya HTC 2 Kampuni ya HTC 2

Kampuni ya Google ambayo ndio watengenezaji wa mfumo wa Android hivi karibuni imefanya makubaliano ya kununua sehemu ya timu ya wafanyakazi zaidi ya 2,000 kutoka kampuni ya HTC kwa dollar za marekani bilioni $1.1.

Sehemu hiyo ya timu kutoka kampuni HTC tayari ilisha anza kufanya kazi na kampuni ya Google kwa kutengeneza simu ya Google Pixel ya mwaka jana 2016 na vilevile timu hiyo ndio inayo tengeneza simu mpya ya Google Pixel 2 inayotarajiwa kutoka October 4 mwaka huu 2017.

Aidha kampuni ya HTC na Google tayari zilisha wahi kuungana na kutengeneza simu mbalimbali kama vile, simu ya kwanza ya Android T-Mobile G1 au HTC Dream, Nexus One ya mwaka 2010, pamoja na Nexus 9 Tablet ya mwaka 2014.

Advertisement

Hii sio mara ya kwanza kwa Google kununua sehemu ya kampuni ya simu kwani mwaka 2011 kampuni ya Google ili nunua kampuni ya Motorola kwa dollar za marekani bilioni $12.5 na baadae mwaka 2014 kuamua kuiuza kampuni hiyo kwa kampuni ya Lenovo kwa dollar za marekani billion $2.91.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Reuters

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use