in

Picha za Simu Mpya za Google Pixel 2 Zavuja Kabla ya Kutoka

Picha za simu kutoka kampuni ya Google zimevuja angali hapa

pixel-2-xl-concept

Kampuni ya Google ambayo ndio watengenezaji wa simu za Pixel hivi karibuni imepata pigo kwa kuvuja kwa picha za simu za pixel 2 ambazo zinasemekana ndio toleo jipya la mwaka huu 2017.

Picha hizo ambazo zimevuja mtandaoni zinaonyesha matoleo yote mawili ya simu za pixel za mwaka huu 2017, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini simu hiyo ni Pixel 2 ambayo itakuwa na ukubwa wa ndani wa GB 4 hadi GB 128, Simu hiyo itauzwa kwa dollar za marekani $649 hadi $749 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,454,409.00 hadi Tsh 1,678,509.00.

Kwa mujibu wa tetesi hizo kwa upande wa simu ya Google Pixel 2 XL simu hii inatarajiwa kuja na kioo cha inch 6 huku ikiwa na ukubwa kuanzia GB 64 ikiwa na price tag ya $849 na nyingine yenye ukubwa wa GB 128 huku ikiwa na bei ya dollar za marekani $949.

Video : Ugumu na Ubora wa Simu Mpya ya LG Wing

Mbali na hayo pia Kumevuja picha ya Mini Google Home ambayo ni spika yenye teknolojia ya Google Assistance ambayo utaweza kuongea nayo kama ilivyo kwenye simu ya iPhone kwa kutumia programu ya SIRI.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : The Next Web

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.