Huenda Samsung Ikasitisha Kutoa Simu Mpya ya Galaxy Note 8

Huenda Samsung ikafanya maamuzi ya kusitisha kutoa simu mpya ya Note 8 ili kufanya maboresho kwanza
Galaxy Note 8 Galaxy Note 8

Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme (Electronics) Samsung huenda ikasitisha kwa mwaka ujao kutengeneza simu yake mpya ya Galaxy Note 8 ili kuangalia namna ya kufanya maboresho ya simu hizo. Yakiwa ni matokeo ya simu mpya ya Galaxy Note 7 kulipuka, Samsung ilipoteza zaidi ya dollar za marekani bilioni $17 (kutokana na mauzo) pamoja na kampuni kupoteza uaminifu kwa baadhi ya watumiaji wa simu zake hizo.

Katika ripoti iliyoandikwa kwenye tovuti ya BGR inasema kuwa huenda kampuni ya Samsung ikaamua kuachana kabisa na utengenezaji wa simu hizo (Note Brand) kwani hivi sasa wateja wa simu hizo wamepoteza uaminifu kabisa na simu hizo pamoja na kampuni ya Samsung kwa ujumla hivyo sio rahisi kwa wateja wa simu hizo kuendelea kutumia matoleo mapya ya simu hizo. Hata hivyo ripoti nyingine kutoka katika tovuti ya Korea ya The Korea Herald, zinasema kuwa kwa sasa kampuni ya Samsung itakua ikizindua simu moja tu kwa Mwaka huku ikiangalia namna ya kuboresha zaidi bidhaa zake na kuangalia jinsi ya kurudisha uaminifu kwa wateja wake waliopotea baada ya matatizo hayo kutokea hapo mapema mwaka huu.

Bado mpaka sasa kampuni ya Samsung haijasema lolote kuhusiana na nini kitafuata baada ya simu hizo kusitishwa, bali Samsung inaonekana inapambana kuhakikisha inarudisha uaminifu kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi simu zake zilizoko sokoni za Samsung Galaxy S7 pamoja na kujitahidi kuwalipa fidia wateja wake watakao endelea kutumia simu kutoka kwenye kampuni hiyo baada ya kurudisha simu za Galaxy Note 7.

Advertisement

Je unadhani ni sawa Samsung wakisitisha kabisa simu zake za Note brand.. ? Tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kuendelea kufuatilia tetesi za kusitishwa kwa Galaxy Note 8 kwa kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram bila kusahau Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use