Samsung Yasitisha Matumizi ya Simu Mpya ya Note 7

Samsung yatangaza kusitisha Matumizi ya Simu yake iliyotoka hivi karibuni ya Note 7
Samung note 7 yasitishwa Samung note 7 yasitishwa

Kampuni ya samsung imetangaza rasmi kusitisha kwa matumizi ya simu zake za Samsung Galaxy Note 7, uhamuzi huo umekuja baada ya samsung kusema kuwa inafanya vipimo tena vya battery za simu hizo ili kuangalia kama simu hiyo inafaa kuingia sokoni.

Hata hivyo haya yamekuja baada ya simu hizo mpya kuonekana zikiwa na tatizo la kulipuka kwa battery baada ya kuwekwa kwenye chaji, baadhi ya nchi ambapo simu hiyo ilikua imefika kumeonakana ripoti kutoka kwa watu mbalimbali wakilaumu simu zao hizo za samsung note 7 kulipuka muda kidogo baada ya kuwekwa kwenye chaji.

Advertisement

Hata hivyo samsung imesema kuwa kwa wale watu wenye simu hizo waepuke kuzichaji na kuto kuzitumia kabisa mpaka simu zingine zitakapo sambazwa, samsung imesitisha usambazaji wa simu hizo kote duniani mpaka hapo itakapo fanya vipimo vya simu hiyo ili kuangalia kama itafaa kurudi sokoni hivi karibuni.

Hata hivyo bado haijajulikana tatizo linalo sababisha kulipuka kwa bettery ya simu hiyo ambayo bado ilikua haijasambaa sana, ili kuenelea kujua zaidi endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use