in

Hizi Ndio Habari Kubwa za Teknolojia kwa Wiki Hii (1/5/2016)

Kama umekosa kusoma habari zote kubwa za teknolojia kwa wiki nzima hii ni kwaajili yako, pia kumbuka hii ni jumapili ya tarehe 1 mwezi 5 mwaka 2016 siku ya mei mosi ambapo Tanzania pamoja na nchi zingine duniani tunasherekea siku ya wafanyakazi duniani, lakini pia kwa upande wa teknolojia tuko pamoja tukiwa tumekukusanyia habari hizi za teknolojia ambazo zimeshika chati kwa wiki nzima kuanzia tarehe 24 hadi siku ya leo yaani tarehe 1 hii yote ni ili kukurahisishia kujua yaliyojiri wiki nzima kwa upande wa teknolojia hivyo kama ulikosa nafasi ya kutembelea blog ya Tanzania tech hii ndo nafasi yako kuzinyaka zote kali za teknolojia zilizojiri wiki hii.

Habari njema kwa wale wanaotumia Adsense Google sasa imeongeza aina ya matangazo ili kukusaidia wewe kujipatia kipato zaidi na kirahisi.

Tazama video ya hizi spika za kichwa (Head Phone) zenye uwezo wa kusoma ubongo wako ili kukupa muziki ambao ubongo wako unaitaji.

Kampuni ya facebook inaendelea tu kukimbiza kuanzia kimapato mpaka idadi ya watumiaji soma ripoti hii mpya ya facebook.

Kwa wapenzi wa samsung habari hii hautakiwi kuikosa kwani samsung wako tayari tena kutoa moja ya bidhaa zao ambazo zilifanyia uzinduzi siku ile ya tamasha la WMC.

Kama unataka kujifunza namna ya kutumia programu ya IDM kwa miaka zaidi ya mitano ukiwa na uwezo wa ku update pamoja na ku-download kwa spidi zaidi soma hii.

Fahamu kuhusu hii project mpya Google ya kutengeneza lensi maalumu ambayo unauwezo wa kuchomwa kama kimiminika na pale inapofika kwenye jicho kubadilika na kuwa lensi maalumu ambazo zina uwezo wa kusaidia tatizo la kutokuona mbali.

Wapenzi wa Microsoft pamoja na Window 10 soma hii inawezekan ni habari njema au ni habari ya mbaya ili kujua soma habari hii.

Jifunze namna ya kutumia programu mbili za whatsapp kwenye simu moja, ujanja huu utakusaidia pale unapokua na namba mbili lakini unanyo simu moja tu hivyo basi soma habari hii upate maujanja.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.