Microsoft Yazuia Google Chrome Kutumika Kwenye Cortana

cortana cortana

Kwa wale wasiojua Cortana ni programu ambayo inafanya kazi sawa na zile program za Google Now na Apple Siri programu hii imetengenezwa ndani ya Window 10 ambapo kazi yake kubwa nikukuleta majibu ya maswali unayo uliza kompyuta yako kama ilivyo programu ya Siri ya Apple.

Hivi karibuni kampuni inayotengeneza Windows yani microsoft imesitisha utumiaji wa search engine kama zile za google na nyinginezo kutumika katika programu yake ya Cortana, hivyo basi kuanzia siku ya jana kila unapoiyambia Cortana itafute kitu katika mtandao tegemea kuona matokeo yako kwenye Browser ya Bing pamoja na Browser inayokuja na programu hiyo yani Edge. Kwa mojibu wa Microsoft mabadiliko haya yanasemekani ni ili kuboresha upatikanaji wa haraka wa vitu katika mtandao kwani programu kama zile za google chrome pamoja na mozila hazina uwezo wa kupata vitu vingi kama ilivyo Bing pamoja na Edge ya Windows 10.

Hata hivyo watu wengi duniani wameonekana kutoku furahishwa na kitendo hicho cha microsoft kuzuia matumizi ya google kwenye programu yake hiyo ya Cortana, hapo awali programu hiyo ilikua ikikuuliza ni browser gani ungependa kutumia kupata matokeo yako lakini sasa programu hiyo imekua ngumu kidogo kutumia, alisema mwandishi wa blog ya habari za teknolojia ya TechCruch ya marekani.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use