Zikiwa zimebaki siku 14 kumaliza mwaka 2017, kampuni ya Apple imetoa list ya programu bora ambazo zimeonekana kufanya vizuri kwa mwaka mzima wa 2017. Kupitia kwa wahariri wa soko la App store hizi hapa ndio programu zilizo fanya vizuri kwenye soko la App Store mwaka 2017.
Kitu kimoja ambacho ningependa ukijue ni kuwa, Apple imechanganya programu zote kwenye list hii yani programu za iPhone, iPad, Apple TV, Apple Watch pamoja na kompyuta za Macbook na iMac.
- Affinity Photo – Kwaajili ya iPad
Programu hii imeingia kwenye list hii kama programu bora duniani kwa mwaka 2017 kwaajili ya ipad, programu hii inafanya kazi kama ilivyo adobe lakini hii ni kwaajili ya ipad, unaweza kuitumia ku-edit picha zako kwa njia ya tofauti kabisa kupitia kifaa chako cha iPad. Kama unataumia iPad hebu ijaribu kisha utupe maoni yako hapo chini.
- Aurora HDR 2018 – Kwaajili ya Mac
Hii nayo ni programu ya ku-edit picha na imeingia kwenye list hii kama programu bora ya kompyuta za Mac duniani kwa mwaka mzima wa 2017.
- Calm – Kwaajili ya iPhone
Calm ni programu kwaajili ya mfumo wa iOS ambayo inakusaidia kuweza kupata afya ya akili kwa ujumla, programu hii itakuwezesha kuweza kupata usingizi kirahisi kupunguza mawazo na wasiwasi pamoja na kukusaidia kuweza kuwa na afya njema ya mwili na akili. Programu hii imeingia kwenye list hii kama programu bora kwa iPhone kwa nchi za Australia, Ireland, New Zealand, USA na United Kingdom
- ChefsFeed – Kwaajili ya Apple TV
Pengine App hii inaweza isiwe na umuhimu mkubwa kwa watanzania lakini ni vyema kuiweka kwenye list hii kama ilivyo onyeshwa na Apple. Na kama ulikua unataka kujua programu hii ina husu nini basi kama lilivyo jina lake programu hii ni kwaajili ya mapishi. Programu hii imekua ni programu bora kwa Apple TV kwa nchi za Canada na USA.
- Ekibo – Kwaajili ya iPhone
Ekibo ni programu bora kwaajili ya vifaa vya iPhone na pia ni programu bora kwaajili ya wale waliopanga kutembelea nchi ya Japan. Programu hii inatumia mfumo wa AI (Artificial Intelligence) kuweza kukupa habari za maeneo mbalimbali unapotembelea nchi ya Japan, App hiyo itakupa habari za njia za kupita, migahawa ya kufikia kwenye eneo ulilopo, hotel bora za kufikia pamoja na mambo mengine mengi yanayohusu wageni. App hii imekua app bora kwa iPhone kwa nchi ya Japan.
- Enlight Videoleap – Kwaajili ya iPhone
Enlight Videoleap ni programu ambayo pengine watu wengi hapa Tanzania wanaijuia hii ni kutokana na umaridadi wake wa kuweza ku-edit video. Programu hii imekuwa bora kwa iPhone kwa nchi za Algeria, Argentina, Austria, Bahrain, Belgium, Bolivia, Brunei, Bulgaria, Cambodia, Canada, Chile China Colombia Costa Rica Croatia Cyprus Czech Republic Denmark Dominican Republic Ecuador ,Egypt, El Salvador Estonia, Finland, France, Germany, Greece, Guatemala, Honduras, Hong Kong Hungary, India Indonesia, Italy, Jordan ,Kuwait, Laos Latvia, Lebanon, Lithuania, Luxembourg, Macau, Malaysia, Malta, Mauritania, Netherlands, Nicaragua, Norway, Oman, Panama Paraguay Peru, Philippines, Poland, Portugal, Qatar Romania, Russia, Saudi Arabia, Singapore, Slovakia Slovenia, South Africa, South Korea, Spain, Sri Lanka, Sweden, Taiwan, Thailand, Tunisia, Turkey, United Arab Emirates, Venezuela, Vietnam, Yemen na nchi nyingine nyingi.
- iTranslate Converse – Kwaajili ya Apple Watch
Programu hii imekua programu bora kwa vifaa vya Apple Watch kwa inchi za Australia, Japan, New Zealand na USA. Programu hii kama lilivyo jina lake ni kwaajili ya kufanya tafsiri kutoka lugha mbalimbali.
- RunGo – Kwaajili ya Apple Watch
Programu hii nayo imekuwa bora kwa vifaa vya Apple Watch kwa inchi ya Canada. Na programu hii inasaidia pale unapokuwa unafanya mazoezi ya kukimbia na itakuwa ikikuonyesha muelekeo wa sehemu mbalimbali kwa kutoa souti ambayo itakuwa ikikuelekeza.
- Tastemade – Kwaajili ya Apple TV
Programu hii imekuwa programu bora kwa inchi za Australia, Japan na New Zealand. Programu hii ni kwaajili ya wapenda mapishi na itakusaidia kutizama video mbalimbali za mapishi pamoja na video za mafunzo ya kupika.
Na hiyo ndio list nzima ya programu bora kwenye soko zima la App Store, kwama unataka kujua list ya programu bora za Apple kwajili ya Game kwa mwaka 2017 unaweza kutembelea ukurasa Huu wa Apple.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
Jinsi ya kuupdate iphone kwenda kwenye ios unayoitaka
Unaweza kufanya hivyo kwa kutafuta kwenye sehemu ya kutafuta utasoma makala kuhusu hivyo.