Imekuwa ni kitu cha kawaida sana siku hizi kwa watumiaji wa simu kuflash simu zao wenyewe, iwe ni kwa sababu ya kuondoa matatizo mbalimbali ya simu husika au kwa kufanya marekebisho fulani.
Kuflash simu imekuwa sio tatizo la kupeleka simu yako kwa mtaalamu, Lakini japokuwa kuflash simu ni kitu cha kawaida na kirahisi lakini bado kuna tatizo juu ya upatikanaji wa programu za kuflash simu mbalimbali za Android.
Sasa kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tumekukusanyia programu maalum za kuflash simu ikiwa pamoja na link maalumu za kudownload programu hizo. Kumbuka, programu hizi zina tofautiana kwenye kila simu hivyo ni muhimu kusoma kwa umakini kabla uja download programu husika.
TABLE OF CONTENTS
Programu za Kuflash Simu
Programu hizi za kuflash simu zina tofauti kwa matumizi hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafuata maelezo ya jinsi ya kutumia programu hizo kwa usahihi ili usije kuharibu simu yako.
Pia ni muhimu kukumbuka kuflash simu yako kunaweza kuharibu baadhi ya mikataba kama vile warranty pamoja na mikataba mingine ya sehemu uliyo nunulia simu yako, hivyo kumbuka kuwa unafanya hivi kwa kutambua madhara ya kuflash simu yako.
SamFirm – Simu za Samsung
SamFirm hii ni programu ya mfumo wa Windows ambayo inatumika kuweza kudownload kwa haraka pamoja na kutafuta firmware za simu za Samsung. Programu hii ni bora sana kwa sababu inasaidia kupata Firmware halisi ya simu yako na pia utaweza kudownload firmware kwa haraka bila kukata kata.
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kuflash simu za Samsung basi unaweza kutumia programu hii kuweza kudownload Firmware ya simu yako.
Odin – Simu zenya Snapdragon
Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Samsung, programu ya Odin ni muhimu wewe kuifahamu. Programu hii inauwezo wa kuflash tablet na simu mbalimbali za Samsung hata zile ambazo ni mpya kabisa kama vile Samsung Galaxy S9 na nyingine kama hizo.
Programu hii ya kuflash simu haiuzwi na ni bure kabisa kutumia unachotakiwa ni kuwa na Firmware ya simu yako ya Samsung ambayo unaweza kuipata hapa, programu ya kuflash simu ya Odin unaweza kuidownload kupitia link hapo chini.
SP Flash Tool – Tecno, Infinix, iTel na Simu za China
Kama wewe ni mtumiaji wa simu za TECNO, Infinix na simu nyingine kama hizo ambazo zinatumia chipset ya MediaTek basi ni vyema kufahamu programu hii ya kuflash simu.
Programu hii inaweza kuflash simu nyingi za kutoka nchini china na pia kama ilivyo programu ya kwanza kwenye list hii programu hii pia ni bure kabisa kudownload na pia ni bure kabisa kutumia, kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa na Firmware ya simu yako ambayo unaweza kuipata hapa. Kwa programu ya SP Flash tool unaweza kupakua kupitia link hapo chini.
Phoenix Suit – Nokia za Zamani
Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu za Nokia za zamani basi ni vyema kufahamu programu hii ya Phoenix Suit, programu hii inauwezo wa kuflash simu mbalimbali lakini zaidi inauwezo wa kuflash simu za Nokia. Unaweza kuipata programu hii bure kabisa kupitia link hapo chini.
Hitimisho
Na hizo ndio programu za kuflash simu ambazo unaweza kutumia kuflash simu yako, programu hizi ni baadhi tu ambazo zimethibitika kuweza kufanya kazi vizuri, kama kuna programu nyingine ambayo itajitokeza siku za karibuni basi moja kwa moja tutaiongeza hapa kwenye makala hii.
Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote hakikisha una jiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia hapa.
samahani kaka nataka kujua jinsi ya kutumia hizo program kwa mfano mimi nina nokia 206 sasa naflash vp kutokana na maelezo yako..?
Hiyo ni Nokia Lumia au..?
Nina Nokia asha 202 nafkash VIP?
Nilikuwa naomba kujuwa jisi ya kuondoa I clud clock kwenye I phone ndug mume kuwa msa ada kwang San n nipo papoja na nyie mupo vizur kwa technology naitaj msa Ada wenu hap nyins ya kutoa I clod clok Kweny I phon
Asante sana
Nashukuru Sana,,ila natumia Huawei chc u 01 je naweza kutumia program ipi hapo,,, na je hio program naidownload kwenye simu ninayotaka kufrash au na download kwenye computer,,asante
Hii ni ya kwenye kompyuta.
Thanks lakini bado sijajua jiyo firmware ni nini pia namna ya kuflash simu
Jinsi ya kuflash simu za Samsung Soma HAPA, Jinsi ya kuflash simu za Tecno Soma HAPA.
Maoni*nawezaje kuflash l9 plus na kuiongezea version??
Asante
Asante Sana
Maoni* naitaji msada wa progr ya ku frashi sim
habari t teck
naomba kupata program ya kuflash bodafone android ili isome line zote
naa inawezekana kjtumia code ku unlock
habari mkuu na shukran kwa elimu unayotupa…….ila nimejaribu kudownload hiyo program ya kuflash simu ya kichina lakini imekataa kufunguka! je kuna tatizo lolote la kiufundi ?
Unaweza kutoa maelezo zaidi..?
Maoni*naomba mnisaidie namna ya kufrash sim bira kutumia box
Mara nyingi hii inategemeana na aina ya simu..
nashukuru san kwa msada wenu lakin mbon hiz progrem m nashindwa kuzi download jaman naomba msadada zaid na maelekezo kwa anae faham.
Asante kwa kuripoti tatizo, tayari tumesharekebisha link zote sasa zinafanya kazi.
Vipi hatua za kufuata iki kuflash Nokia kwa phoenix suit mkuu
Kaka wengine hatujui kiingereza
VIP kaka una faili la Tecno w3
asante
Nina simu ya huwawei y520-u22 nijaribu kuiflashi inagoma file nimedownload lakini imeshindikana maanake file za simu zinaandika unfortunately stopped nisaidie shida yake niipi? au nitumie njia gani ili ipone
Kikubwa mimi naitaj msa ada wen kujua mambo mengi sana juu ya kompyuta na ku download progarm
Lakin pia kompyuta yangu inasumbua sana maana inadai ku activate lakin Sijajua ku download kmspico nakila nikijaribu kudownload kwenye Sm lakin nikiweka kweny kompyuta inagoma kufanya kazi na kompyuta yangu inasumbua sn hadi Kwasas kuna badh y program azifany Kaz naitaj San msa Ada web
Naitaji kuflashi simu ndogo ya kipadi aina ya kgtel nifuate hatua zipi