in

Jinsi ya Kuflash Simu za Samsung za Aina Zote

Kuflash simu za Samsung

Kama unafikiria ku update simu yako ya Samsung kuna njia nyingi za kufanya ikiwemo njia maalumu ya kutumia Samsung kies, lakini wengi wetu hua pia application hiyo ya Samsung kies haifanyi kazi pia kwa hiyo unabakia na njia moja tu yaku update simu yako, zifuatazo ni njia za ku-flash au ku-update Samsung original.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

VITU UNAVYOITAJI

  1. Utaitaji computer yenye uwezo wa kawaida inayotumia Window 7, 8 au 10
  2. Waya wa USB Original wa simu yako.
  3. Pia utaitaji Internet at list GB 1 au zaidi.
  4. Utaitaji Software ya Computer iitwayo Odini Download Hapa
  5. Pia kwa uhakika download na Install Driver za Samsung kwenye computer yako. Download Hapa.
  6. Download Firmware ya zimu yako Download Hapa

NOTE : KUMBUKA KUZIMA APPLICATION YA SAMSUNG KIES KABLA UJAWASHA ODINI

NAMNA YA KU-INSTALL AU KU-FLASH

  1. Download Odin 3.09 kwenye Computer yako hakikisha ni odin 3.09 (Matoleo mengine ya program hii hua si bora kwa Samsung. Unaweza ku search kwenye google model ya simu yako kisha andika neno odin)
  2. Extract au fungua file ZIP na chagua extract.
  3. Hakikisha Samsung Kies Imezimwa kabisa kwenye computer yako.
  4. Zima simu yako na uhakikishe imezima kabisa, kisha bonyeza vibonyezo “Power+Volume Down+Home” kwa pamoja ilikuweka simu kwenye “Download Mode”.
  5. Connect Simu yako kwenye PC au Computer kwa kutumia Cable Orignal ya simu yako.
  6. Right Click kwenye Odin kisha select “Run as administrator
  7. Hivi ndivyo inavyotakiwa kuonekana.
  1. Kuna sehemu iliyoandikwa ID:COM inayopatikana upande wa kushoto juu kwenye window ya Computer yako sehemu hiyo itabadilika kuwa rangi ya blue kama simu yako itakua imekua connected vizuri.
  1. Bonyeza “AP” kisha weka file liitwalo “.md5” kutoka kwenye Mahitaji Namba 6.
  1. Kumbuka usije ukaweka chochote kwenye sehemu ilioandikwa “PIT” pia hakikisha sehemu iliyoandikwa “Re-Partition” Hijawekwa tiki. Sehemu hii inapatikana upande wa kushoto chini ya Opition
  1. Ukisha maliza bonyeza “Start” kuanza ku-flash simu yako.
  1. Usiguse USB au Simu yako mpaka itakapo jiwasha yenyewe.

Kwa Maelezo zaidi fuatilia video hapo juu na pia kama unaitaji msaada zaidi nenda kwenye facebook page ya Tanzania techna uliza swali lako tutakusaidia.

KUMBUKA KUA MAKINI SANA UNAPO FLASH SIMU YAKO NA JUA KUA UNAWEZA UKAHARIBU SIMU YAKO KABISA, KWA HIYO KUWA MAKINI.

Jinsi ya Kuflash Simu za Samsung za Aina Zote
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

16 Comments

  1. Hi wakubwa…nina tatzo kdg cm yangu haisomi mtandao kabisa na nme restore kila kitu mpk factory reset ila bado tu….nini tatzo wakuu coz mtandao unasoma ila hai function kupiga cm wala nn na ukipiga inaandika NO REGISTERED NETWORK…MSAADA HAPO SIMU NI SAMSUNG GT-I93001