Soko la programu za Android Play Store linakuwa kilasiku huku watu wakiwa wana endelea kuweka programu mpya kila siku kiasi cha kufanya kwa sasa soko hilo kuwa na programu zaidi ya milioni 2.8 na namba hiyo ikizidi kuongezeka kila siku. Ndio maana Tanzania Tech tunakusaidia kujua programu mpya za mwezi ili kukurahisishia kujua ni programu gani ambayo pengine itaku rahishia maisha yako ya kila siku.
- Airtel Money – Recharge & Pay
Hivi karibuni kampuni ya Airtel nayo imeweka toleo jipya la programu ya Airtel Money unaweza kudownload programu hiyo ili kujua maboresho, kwa mujibu wa Google programu hiyo imewekwa tarehe March 7, 2017.
- M-Pesa
Wengi wetu tunaijua Vodacom kwa namna moja au nyingine kama unaifahamu basi lazima utakua unaijua pia M-Pesa basi hii ndio programu yake ambayo itakuwezesha kutuma na kupokea pesa kwa urahisi zaidi. App hii imezinduliwa tarehe March 31, 2017.
- Wasafi
Programu kwaajili ya kupakua nyimbo za wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania kujua zaidi kuhusu programu hii bofya hapa, kwa mujibu wa Google Play Store App hii imezinduliwa March 26, 2017.
- Perfect 255
Kama unataka habari za mastaa wa bongo pamoja na wengine kutoka nje ya nchi basi hii ndio app mpya kwaajili ya hayo, app hii imezinduliwa March 16, 2017.
- CloudsFm Top20
Hii ni app mpya ya kuchagua nyimbo ili iweze kuingia kwenye kumi bora app hii imezinduliwa hivi karibuni kwa mujibu wa Google App hii imezinduliwa Tarehe March 1, 2017.
- Paul Makonda
Programu ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa na lengo la kuleta taarifa mbalimbali kuhusu yeye, programu hii imeinduliwa tarehe March 5, 2017 kwa mujubu wa Google.
- Super Mario Run
Kwa kumalizia hii ni kwa wale wapenzi wa game mwezi huu game mpya ya Super Mario Imetoka kwenye mfumo wa Android Game hii imezinduliwa tarehe March 22, 2017.
Na hizo ndio baadhi tu ya programu ambazo zimeingia kwenye Play Store, kumbuka kuwa hizi sio programu zote bali hizi ni zile ambazo zimetafutwa sana kwenye soko la Play Store hivyo kama hujaona programu yako usijali unaweza kutuma programu hiyo ili tuiongeze kwenye list hii kupitia hapa.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.