Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tigo Pesa na M-Pesa Zapata Uthibitisho Kutoka Shirika la GSMA

Je uthibitisho huo unafaida gani kwa watumiaji wa Simu na teknolojia kwa ujumla..?
Tigo Pesa na Mpesa Tigo Pesa na Mpesa

Wakati matumizi ya simu za mkononi yakiongezeka kwa kasi hapa Tanzania, Huduma za kutuma na kupokea pesa zimekuwa ni nguzo muhimu sana miongoni mwa watanzania. Ni wazi kuwa tukiongelea swala la kutuma na kupokea pesa ni lazima tutazitaja huduma za kutuma na kupokea pesa za Tigo Pesa na M-Pesa kwani huduma hizo zimekua zikiongoza sana kwa hapa Tanzania.

Sababu hizo na nyingine ndio zilizofanya kampuni za Tigo Tanzania (Millicom Group) na Vodacom Tanzania kupokea uthibitisho wa kimataifa ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’. Uthibitisho huo maana yake ni kuwa kampuni hizo zimeweza kutoa huduma salama, kwa uwazi, kwa kuaminika, kiuthabiti na kwa kusimamia haki za wateja na kuzuia miamala ya kihalifu.

Advertisement

Kwa mujibu wa Shirika hilo la kimataifa la GSMATigo Tanzania (Millicom Group) na Vodacom Tanzania ni moja kati ya watoa huduma za kifedha kwa simu za mkononi wa kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huu kutoka GSMA.

Kwa wale ambao hawajui ‘GSMA Mobile Money Certification’ ni nini .? Basi ningependa ufahamu kuwa, GSMA Mobile Money Certification’ ni mkakati mpya wa kimataifa unaolenga kuleta huduma za kifedha salama, wazi na thabiti zaidi kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi duniani kote.

Huku kukiwa na zaidi ya akaunti 690 milioni za fedha kwa simu za mkononi duniani, sekta ya simu za mkononi inaboresha maisha duniani na imewezesha mamilioni ya watu wasiokuwa na akaunti za benki kufikiwa na huduma rasmi za kifedha, Lakini je hii inatosha..?. Kwa upande wangu naona bado haitoshi kwani kuna huduma nyingi za kifedha hazija wezeshwa na makampuni haya yanayo simamia huduma hizi za kutuma na kupokea pesa kwa kutumia simu za mkononi kwa hapa Tanzania

Moja ya huduma hizo ni pamoja na huduma muhimu kama za kufanya manunuzi mtandaoni, urahisi wa kutuma pesa au kupokea pesa kutoka mtandaoni kuja kwenye huduma za simu za mkononi na huduma nyingine kama hizo. Pamoja na kuwa vigezo vilivyotumika katika utoaji wa uthibitisho huo ni kuangalia zaidi huduma bora zilizoko sasa, lakini bado naona kama ni muhimu pia uthibitisho huo ungeangalia pia teknolojia kwa ujumla ili kuweza kutoa uthibitsho mzuri zaidi kwa kampuni zinazo endana na kasi ya teknolojia.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Tigo, GSMA imebainisha kuwa vigezo vinavyotumika kutoa uthibitisho huu vinazingatia viwango vya ubora wa kimataifa katika utoaji huduma za kifedha. Kabla ya kupokea uthibitisho huo, kila mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu za mkononi sharti afikie asilimia 100% ya vigezo vilivyowekwa. Watoa huduma wanaopokea uthibitisho huu ni wale tu waliofanikiwa kuonesha kuwa hatua za uendeshaji wa biashara zao ni miongoni mwa zile zilizo bora, zinazoaminika na kuwajibika zaidi katika mfumo mzima wa utoaji huduma za kifedha duniani.

Kama unavyoona hakuna mahali palipo zingatia sana teknolojia, au hata kama walizingatia sio kwa viwango vile vinavyo hitajika na watumiaji wa huduma hizi. Hivi karibuni Safaricom ya Kenya ilitangaza ujio wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia PayPal na kuja kwenye huduma za M-Pesa, ikiwa pamoja na huduma ya kuwawezesha watumiaji wa Android kuweza kulipia App kwa kutumia M-pesa.

Huduma zote hizi ndio mfano wa teknolojia inayotakiwa kuangaliwa na mashirika ya kimataifa kama GSMA kwani hata hivyo shirika hilo ndilo linalo simamia maswala makubwa ya teknolojia za simu za mkononi ikiwa pamoja matamasha makubwa ya teknolojia duniani kama Mobile World Congress na mengine kama hayo. Hivyo ni wazi kuwa pamoja na kampuni hizo kupokea uthibitisho huo bado zinahitajika kufanya kazi za ziada katika kuhakikisha zinaendana na kasi ya teknolojia kama nchi nyingine.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use