Huu Hapa Muonekano wa Simu za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus

Muonekano wa kwanza wa simu mpya za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus
Huu Hapa Muonekano wa Simu za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus Huu Hapa Muonekano wa Simu za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus

Ikiwa zimebaki siku chache kwa simu mpya za Samsung Galaxy S9 kutoka rasmi, huku kwenye mtandao nako kumefurika picha na video mbalimbali ambazo watu wamekua wakibainisha muonekano wa simu hizo kabla ya kutoka kwake.

Katika kufanya uchunguzi wa kina pamoja na kusoma baadhi ya sifa za simu hizo mpya sasa tunakuletea picha na video hii ambayo inaonyesha muonekano wa simu hiyo jinsi itakavyokuwa.

Picha hiyo hapo juu ni muonekano wa nyuma wa simu za Samsung Galaxy S9 na Galaxy S9 Plus, picha hiyo imepatikana kutoka mtandao wa maarufu wa Weibo wa nchini china. Mtandao huo unasifika kwa kuvujisha picha mbalimbali za simu kabla ya kutoka kwake.

Advertisement

Kwa mujibu wa mtandao huo simu ya Galaxy S9 Plus ambayo inategemewa kuja na kamera mbili kwa nyuma inategemewa kuja na processor za Qualcomms Snapdragon 845 au Exynos 9810 lakini pia simu hiyo inategemewa kuja na RAM ya GB 6 huku ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128 pamoja na mfumo mpya wa uendeshaji wa Android 8.0 Oreo.

Na huo ndio muonekano wa simu mpya ya Samsung Galaxy S9 na S9 Plus simu ainayotarajiwa kutoka mapema mwezi wa pili na inategemewa kuja kwa matoleo matatu ya Galaxy S9, Galaxy S9 Plus pamoja na Galaxy S9 Mini.

Nini maoni yako kuhusu muonekano huu.. Tuambie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use