Kampuni ya Tecno hivi leo imezindua simu yake mpya ya Tecno Phantom X, simu ambayo ni toleo jipya la simu za phantom ambazo hapo mwaka jana hazikuweza kuzinduliwa.
Kwa mwaka huu, Tecno imezindua toleo la Phantom X ambalo ni premium na ukweli simu hii kwa sasa inakuja na sifa za tofauti pengine kuliko simu zote za Tecno ambazo unazifahamu kwa sasa. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja tukangalie sifa za simu hii mpya kutoka Tecno.
Kwa kuanza Tecno Phantom X inakuja na kamera tatu kwa nyuma, huku ikiwa na kamera kuu ya Megapixel 50, kamera nyingine mbili zinakuja na Megapixel 13 na nyingine ya mwisho ikiwa na Megapixel 8. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera mbili za Selfie zenye Megapixel 48 na Megapixel 8.
Mbali na kamera, Tecno Phantom X inakuja na kioo cha Super AMOLED chenye ukubwa wa inch 6.7. Kioo hicho pia kinakuja na resolution ya hadi pixels 1080 kwa 2340. Simu hii pia inakuja na refresh rate ya hadi 90Hz. Mbali na hayo kioo hicho kina ulinzi wa Gorilla Glass 5.
Tofauti ya kioo cha mbele, Tecno Phantom X pia imetengenezwa kwa Glass ambayo pia imetengenezwa kwa Gorilla Glass 5.
Kwa upande wa sifa za ndani, Phantom X inakuja na uhifadhi wa ndani wa GB 256 huku ikisaidiwa na RAM ya hadi GB 8. Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili kama simu hii inaweza kutumia memory card.
Tukiachana na uhifadhi wa ndani wa simu hii, Phantom X inakuja na processor yenye chipset ya Mediatek Helio G95, ambayo inakuja na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core (2×2.05 GHz Cortex-A76 & 6×2.0 GHz Cortex-A55). Kwa ajili ya Graphics simu hii inakuja na GPU ya Mali-G76 MC4.
Mbali na hayo simu hii inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo ipo chini ya kioo, ikiwa pamoja na sensor nyingine za accelerometer, gyro, na proximity. Phantom X pia inakuja ikiwa na Radio FM pamoja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
Kwa upande wa Battery, Tecno Phantom X inakuja na battery ya 4700 mAh, battery ambayo inachajiwa na chaja yenye uwezo wa hadi 33W, huku Tecno ikidai kuwa simu hii inaweza kujaa chaji kutoka asilimia 0 hadi 70 kwa dakika 30.
Simu hii inakuja kwa rangi mbili za Starry Night Blue, na Monet Summer. Kuhusu upatikanaji simu hii inategemewa kuanza kupatikana rasmi mwezi July. Kwa hapa Tanzania bado hakuna tarehe kamili ila unaweza kutembelea tovuti yetu ya price in tanzania kujua zaidi kuhusu simu hii mpya.