in

Apps Nzuri za Kufanya Meseji za WhatsApp Zijitume Zenyewe

Kama unataka kutuma meseji za WhatsApp kwa muda maalum bila kushika simu soma hii

Apps Nzuri za Kufanya Meseji za WhatsApp Zijitume Zenyewe

Ni kweli kwamba wote kama binadamu huwa tunatabia ya kusahau, lakini kwa sababu ya teknolojia ni wazi kuwa kwa sasa swala la kusahau limeanza kupungua hasa ikija kwenye maswala haya ya kutuma meseji kwa muda maalum.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha apps nzuri ambazo zinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine kuto kusahau kutuma WhatsApp meseji ambayo ulikuwa unatarajia kutuma baadae kwa muda fulani. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao labda unataka kumkumbusha mtu deni lako au labda unataka kumtakia mkeo heri ya siku ya kuzaliwa basi app hizi zita kusaidia sana usisahau kutuma meseji hiyo.

Kumbuka Apps hizi ni kwa ajili ya simu za Android, kwa watumiaji wa simu za mfumo wa iOS endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuja na list hiyo hivi karibuni.

SKEDit Scheduling App

SKEDit ni app nzuri sana ya Android ambayo inakusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe, mbali ya WhatsApp app hii inaweza kufanya mambo mengi sana kama vile kusaidia status kwenye mtandao wa Facebook zijiposti zenyewe, kusaidia barua pepe ijitume yenyewe pamoja na meseji za kawaida SMS nazo unaweza kufanya zijitume zenyewe kupitia App hii.

Apps za Kufuatilia Michuano ya (UEFA) Champions League

AutoResponder for WA

AutoResponder for WA ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya kusaidia meseji za WhatsApp kujituma zenyewe, app hii ni nzuri sana kwa sababu hii inakusaidia kujibu meseji za watu bila hata wewe kuangaika kufungua app ya WhatsApp. App hii inauwezo wa kusoma maneno kadhaa ambayo utakuwa umeyaandika ndani ya app hiyo na pale mtu atakapo andika maneno hayo kama ujumbe wa WhatsApp basi atapata majibu ambayo umeandika awali.

WhatsAuto – Reply App

WhatsAuto - Reply App
Price: Free+

WhatsAuto ni app nyingine ambayo haina tofauti sana app iliyopita, app hii nayo itakusaidia kujibu watu meseji pale watakapo kuwa wamekuandikia ujumbe fulani kwenye WhatsApp. Kumbuka ni lazima kuandika sentensi ambayo unataka ijibiwe kwa kutumia app.

Autoresponder for WA Auto-reply SMS Business Card

Autoresponder for WA Auto-reply SMS Business Card ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa simu za Android, app hii nzuri kwa sababu inakusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe lakini pia inakusaidia kutuma Business Card kupitia SMS app hii ni nzuri sana kwa wafanya biashara hivyo kama wewe ni mfanya biashara nakushauri jaribu app hii.

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

AutoResponder for FB Messenger

App ya mwisho kwenye list hii na tofauti kidogo kwani haiusiani na WhatsApp, App hii itakusaidia sana kama wewe ni mtumiaji wa Facebook Messenger. Utaweza kuwajibu watu meseji zako kwa haraka kupitia Facebook Pia utaweza kufanya meseji hizo zijitume zenyewe bila wewe kufungua app ya Messenger.

Na hizo ndio apps nzuri ambazo zinaweza kusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe, kumbuka app hizi ni kwa ajili ya Android na kama unatumia mfumo wa iOS basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuja na list ya App hizo kwa mfumo huo. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua App za kusaidia kutengeneza Beat kupitia simu yako ya Mkononi ya Android.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.