Google Yataja Apps Zilizoshinda Tuzo ya Google Play Awards 2019

App bora kwenye soko la Play Store kwa mwaka 2019
Google Yataja Apps Zilizoshinda Tuzo ya Google Play Awards 2019 Google Yataja Apps Zilizoshinda Tuzo ya Google Play Awards 2019

Wakati mkutano wa Google I/O 2019 ukitegemewa kuanza rasmi siku ya leo huko nchini Marekani, Google kupitia soko lake la programu za Android la Play Store imetaja na kutoa tuzo kwa Apps bora kwenye soko hilo zilizo shinda tuzo za Google Play Award 2019.

Mashindano hayo ya Google Play Award yanahusisha wabunifu wa programu na programu zenyewe ambazo zinakuwa kwenye vipengele zaidi ya tisa, huku mwaka huu Google ikiwa imeongeza vipengele vingine kama vile Most Inventive, Best Living Room Experience pamoja na Most Beautiful Game.

Google Yataja Apps Zilizoshinda Tuzo ya Google Play Awards 2019

Advertisement

Zifuatazo ndizo apps ambazo zimefanikiwa kupata tuzo ya kwa mwaka huu 2019 kupitia soko la Google Play Store, kumbuka Apps zote tulizo angalia kwenye list hii ni zile apps ambazo zina wezekana kutumika kwa nchi za Africa na Tanzania kwa ujumla, zipo apps ambazo hazipo kwenye list hii lakini nazo pia zimeshinda tuzo hizo kwa mwaka huu 2019.

Woebot ni app iliyoshinda tuzo kwa kuwa app bora kwenye kipengele cha Well-Being App, app hii inakupa uwezo wa kuchat na robot ambayo itakupa msaada wa kiakili pindi utakapokuwa na tatizo. App hii inakupa fursa ya kuweza kubadilisha maisha yako kupitia afya ya akili na tabia njema.

Envision
Price: Free

Envision AI ni app nyingine ambayo imepewa tuzo na Google kwa kuwa app bora kwenye kipengele cha Best Accessibility Experience. App hii inatoa uwezo kwa watu wasio ona vizuri kuweza kusoma, kujua sura za watu pamoja na kufanya mambo mengine mbalimbali.

SHADOWGUN LEGENDS ni game ambayo imeshinda tuzo kwenye kipengele cha Most Beautiful Game. Game hii kweli ni nzuri na inahisisha mapigano baina ya robot mbalimbali.

Neverthink ni app nyingine kwenye list ya Google ambayo nayo imeshinda tuzo kwenye kipengele cha Best Living Room Experience. App hii inakupa uwezo wa kuangalia video za YouTube kutokana na aina ya video unazopenda bila kukata kata kutoka video moja kwenda nyingine.

Canva ni app nyingine ambayo imeshinda tuzi kwenye kipengele cha Standout Build for Billions Experience, App ya Canva inakupa uwezo wa kutengeneza picha kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile mitandao ya kijamii pamoja na vitu mbalimbali.

Slowly ni app nyingine iliyoshinda tuzo kwenye kipengele cha Best Breakthrough App. App hii inakupa uwezo wa kutafuta marafiki kwa njia ya kuandikiana barua kama ilivyokuwa zamani, kupitia app hii utaweza kukutana na watu ambao wanafanana na wewe tabia na baadhi ya vitu.

MARVEL Strike Force nayo ipo kwenye list hii kama app bora kwenye kipengele cha Best Breakthrough Game. Game hii kama bado hujajua inakupa uwezo wa kuchagua kikosi cha wapiganaji kutoka kwenye filamu za Marvel na utaweza kupiganisha wahusika hao na wahusika wengine.

Na hizo ndio apps ambazo zimeshinda tuzo ya kuwa Apps bora kwenye soko la Play Store kwa mwaka 2019, kama unataka kujua list kamili unaweza kusoma list hii kupitia tovuti ya Google HAPA.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use