Kampuni ya Xiaomi Kufungua Duka la Kwanza Afrika Mashariki

Hatimaye sasa utaweza kununua simu mpya za Xiaomi kwa urahisi
Kampuni ya Xiaomi Kufungua Duka la Kwanza Afrika Mashariki Kampuni ya Xiaomi Kufungua Duka la Kwanza Afrika Mashariki

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kieletroniki yenye makao yake makuu huko nchini China Xiaomi, hivi karibuni iltangaza kuja rasmi Afrika mashariki na kuanza rasmi kuuza bidhaa zake kwa mara ya kwanza. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, hatimaye ahadi hiyo imetimia na Xiaomi imetangaza kufungua duka lake la kwanza hapa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa tweet iliyotumwa na akaunti ya Xiaomi ya nchini Kenya, Kampuni hiyo inatarajia kuuza bidhaa zake za TV, simu, spika za bluetooth pamoja na Smartwatch (saa janja) kwenye duka lake hilo ambalo litafunguliwa rasmi mwezi wa tano (May) mwaka huu 2019 huko nchini Kenya.

Xiaomi ni moja ya kampuni zenye kuuza simu bora kwa bei nafuu sana, hivi karibuni kampuni hiyo ilizindua simu mpya ya Redmi 7 ambayo ilikuwa inakadiriwa kuuzwa kwa takribani Tsh 250,000 za kitanzania. Mbali na hayo Xiaomi pia inauza TV za kisasa kwa bei nafuu sana TV zinazo semekana kuwa na ubora wa hali ya juu.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za kampuni hiyo kufungua duka lake au sehemu ya kampuni hiyo hapa Tanzania, kwa sasa bidhaa za Xiaomi kama vile TV pamoja na Smartphone zinapatikana kupitia soko la Jumia. Hadi hapo tutakapo pata taarifa zaidi kuhusu ujio wa kampuni hiyo hapa nchini hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa kwa wakati.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use