in

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni kwa Kutumia WhatsApp

Tengeneza pesa huku unatumia mitandao yako ya kijamii

Jinsi ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni kwa Kutumia WhatsApp

Ni kweli imezoeleka kwamba, kama unataka kutengeneza pesa mtandaoni ni lazima uwe na tovuti au (Website) au Application ndio uweze kufanya hivyo, lakini siku hizi kwa sababu ya uwepo wa mitandao ya kijamii pamoja na programu kama WhatsApp basi kutengeneza pesa mtandaoni imekuwa ni rahisi sana kuliko hapo awali.

Sasa kuliona hili leo nimekuletea njia mpya kabisa ya kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia programu yako ya WhatsApp, Njia hii ni rahisi lakini inahitaji ufanisi zaidi ili kusudi uwezo kuanza kuona mafaniko mengi zaidi.

Lakini pia ili kuweza kufanya hatua hii inakuitaji kuwa na Smartphone na pia uwe na Internet bila kusahau programu ya WhatsApp ambayo nina hakika unayo kwenye simu yako hivi sasa. Kama tayari unavyo vitu hivyo basi utakuwa huko tayari kwenda kwenye hatua za awali za kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia programu ya WhatsApp.

Kutengeneza Pesa Mtandaoni kwa Kutumia PropellerAds

PropellerAds ni moja kati ya kampuni nyingi zenye mfumo wa tofauti wa kutengeneza pesa mtandao, kampuni hii inatoa ruhusa kwa watumiaji wa internet kuweza kutengeneza kipato kwa kuweka matangazo kwenye tovuti au kwa kutumia njia za kisasa kama hii ambayo nitakuelekeza.

Hatua za Kufuata

 • Kwa Kuanza unatakiwa kuwa na Internet kwenye simu yako kisha ingia kwenye tovuti ya propellerads.com kwa kubofya link hapa. Baada ya hapo utapelekwa kwenye sehemu ya usajili jaza taarifa zako kwa usahihi.
 • Baada ya kujaza data zako za muhimu hakikisha unaweka barua pepe ambayo inafanya kazi kwani utakuwa unatumia barua pepe hiyo mara zote pia endapo utasahau barua pepe hiyo hutoweza kulipwa pesa ulizozipata.
 • Baada ya kujisaji kwa ukamilifu sasa utaingia kwenye profile yako kisha upande wa kushoto bofya Menu ya vimikato vitatu kisha utaona sehemu imeandikwa Smart Links, bofya hapo kisha endelea kufuata maelezo mengine hapo chini.

YALIYOMO

Tovuti Inayotengeneza $100 Kila Mwezi (Bila Kufanya Chochote)

Mabadiliko

 • Baada ya kubofya hapo utapelekwa kwenye ukurasa maalum, kisha bofya mahali palipo andikwa Direct Link baada ya hapo bofya sehemu inapatikana juu upande wa kulia iliyoandikwa Create Direct Link, baada ya kubofya sehemu hiyo utapelekwa kwenye uwanja maalum ambapo utachagua Jina la link hiyo kisha bofya Get Tag.
 • Chagua kwanza sehemu ya Create Smart Link, na kisha ndipo uchague aina ya link ambayo utapendelea kutumia kutengeneza pesa mtandaoni kupitia WhatsApp.
 • Baada ya kubofya sasa utaweza kuiona link yako na utaweza kubofya sehemu ya Copy iliyoko mbele ya link yenyewe. Baada ya kuchukua link yenyewe ni wakati wa kuanza kutengeneza kipato kwa kushare link hiyo kwenye magroup yako ya WhatsApp pamoja na mitandao mingine ya kijamii.

Kumbuka link hii inafanya kazi kisasa na inauwezo wa kuonyesha vitu mbalimbali pale mtu anapo bofya, link hii huonyesha matangazo mbalimbali na hivyo kufanya uweze kulipwa kutokana na watu kubofya link yako. Pia kama unatumia mitandao ya kijamii kama Instagram unaweza kuiweka Link hiyo kwenye Bio yako ili uweze kupata pesa pale mtu atakapo bofya link hiyo.

Biashara Ngumu Kufanya Mtandaoni Hapa Tanzania (2020)

Sasa unaweza kupata pesa zaidi kutokana na aina ya watu wanao bofya link yako, kwa mfano pale watu 1000 au zaidi wanapo bofya link yako unaweza kulipwa kiwango cha chini cha dollar $90 hadi $100 na hii hutegemeana na watu wanao bofya link hiyo wako nchi gani.

Kama unayo magroup mengi zaidi ya WhatsApp basi hii itakuwa ni njia rahisi zaidi kwa wewe kuweza kupata pesa nyingi zaidi wakati unatumia programu yako ya WhatsApp.

Guys njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100 na nimefundisha watu kadhaa ambao wameweka link hii kwenye Bio za Instagram na Sasa wanategeneza pesa hadi kiasi cha dollar $100 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Tsh 230,000 kwa kutumia tu programu za mitandao ya kijamii. Unaweza kujaribu sasa njia hii kwani haikupotezei muda wala haikugaribu kitu chochote.

Makala Imeongezwa:

Makala imeongezwa kuonyesha unatakiwa sasa kuchagua Direct Link na sio Smart Link kwani Smart Link imeondolewa kwenye Propeller Ads.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 51

Toa Maoni Hapa

            Toa Maoni Hapa

            Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.