in

Je Wajua WhatsApp Sasa Inapatikana kwa Lugha ya Kiswahili

Sasa unaweza kutumia programu ya WhatsApp kwa lugha ya Kiswahili

WhatsApp kwa Kiswahili

Programu ya WhatsApp ni moja kati ya programu zinazotumiwa na watu wengi sana kwa sasa, programu hii imewezesha watu kuwasiliana kwa urahisi, iwe ni watu kutoka nje au ndani ya Afrika. Kurahisisha mawasiliano hivi karibuni mitandao mbalimbali ya kijamii imeanza kutambua Kiswahili kama lugha rasmi ya kuwasiliana ndani ya mitandao hiyo.

Baada ya kusikia kuwa Twitter inasemekana kutambua Kiswahili kama lugha rasmi, Sasa WhatsApp nayo imekuja na kiswahili kama lugha rasmi ya kutumika ndani ya programu hiyo.

Kupitia programu ya WhatsApp ya Android sasa unaweza kubadilisha lugha ya programu hiyo moja kwa moja na utaweza kutumia programu hiyo ikiwa kwenye lugha adhimu ya kiswahili. Kama unavyona kwenye picha hapo chini maneno yote kwenye programu hiyo yamebadilika na kuwa kwa lugha ya Kiswahili.

  • Jinsi ya Badilisha App ya WhatsApp Kuwa ya Kiswahili

Kama ulikuwa unataka kubadilisha programu yako ya WhatsApp ya Android kuwa ya kiswahili unaweza kufuata hatua hizi. Kwanza hakikisha una update app yako ya WhatsApp kisha baada ya hapo fungua App hiyo kisha ingia kwenye Settings > Chats >  App Language iko juu kabisa, kisha chagua Kiswahili. Kama unataka kurudisha App ya WhatsApp kuwa ya Kingereza bofya Mpangilio > Soga > Lugha ya programu, badilisha na weka Lugha ya simu.

Kwa upande wa iOS bado hatujafanikiwa kupata jinsi ya kubadilisha lugha kwa mfumo huo, tutaendelea kutafuta sehemu hii na uhakika itakuja kwa watumiaji wa iOS siku za Karibuni.

Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19

Hii ni hatua nzuri sana kwa Tanzania na nchi nyingine zinazotumia Kiswahili kwani siku sio nyingi mitandao mingine mikubwa itakuwa na uwezo wa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ndani ya mitandao hiyo. Kama umefanikiwa kubadilisha lugha tuambie umeonaje kutumia programu hiyo kwa Kiswahili..? Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 3

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.