Apps# 14 Jaribu App Hizi Nzuri Kwenye Simu ya Android

Furahia app hizi nzuri kwenye simu yako ya Android
App nzuri za Android App nzuri za Android

Karibuni tena kwenye makala nyingine ya App nzuri za Android, kama kawaida hapa tunapata nafasi ya kuweza kuangalia Apps nzuri za android ambazo zinaweza kufanya matumizi ya simu yako ya Android kuwa rahis. Kama wewe ni mgeni napenda kukukaribisha sana na kama wewe ni msomaji wa makala hizi basi kumbuka unaweza kusoma makala nyingine kama hizi za app nzuri kwa kubofya link inayopatikana mwishoni mwa makala hii.

1. Phone Schedule – Call, SMS, Wifi

Hii ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kuweza kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako bila kushika simu yako, unaweza kuset app hii iweze kutuma meseji kwa muda flani, pia unaweza kuset app hii ikusaidie kupiga simu kwa muda flani pamoja na kufanya mambo mengine kama kuwasha muziki kwenye simu yako na mambo mengine kama hayo.

2. Shout

Shout
Price: Free

Shout ni app nyingine nzuri sana ya kujaribu kwenye simu yako ya Android, App hii itakusaidia kugeuza simu yako kuwa MIC, yaani kama imetokea unataka kufanya jambo lolote linalo hitaji Mic basi unaweza kutumia app hii kwa urahisi zaidi. Chomeka Mic kwenye tundu la headphone la simu yako, kisha washa app hii na hapo utakuwa tayari umefanikisha kupata Mic kwa kutumia simu yako.

Advertisement

3. Pro Search

Pro Search
Price: Free

Pro Search ni app nyingine ambayo ni nzuri sana, App hii inakusaidia kuweza kutafuta vitu kwa wakati mmoja, kwa mfano kama unatafuta neno “maujanja”, app hii itakusaidia kuweza kupata maujanja mbalimbali kupitia YouTube, Facebook pamoja na Google kwa pamoja, yaani huna haja ya kutafuta neno hilo kwenye tovuti za Google na Youtube kwa wakati tofauti, bali app hii itakusaidia kutafuta neno hilo moja kwenye tovuti zote na kurahisisha kazi ya kutafuta kwa nyakati tofauti.

4. Voicera

Voicea A.I. Note Taker

Voicera ni app nyingine nzuri kwenye list hii, app hii itakusaidia kuweza kurekodi maongezi fulani kwa usahihi na pia kizuri zaidi kuhusu app hii ni kuwa, itakusaidia kuweza kuandika maongezi hayo. Kama wewe umekuwa ni mtu wa kudhuria mkutano au makungamano mbalimbali basi app hii ni nzuri sana kwako ijaribu kwenye simu yako ya Android.

5. GlassWire Data Usage Monitor

GlassWire ni app nzuri sana kwa wale wanao jikuta bando linaisha bila kujua, App hii itakusaidia kujua ni app gani inatumia data kwa muda gani, pia itakusaidia kuweza kuset ni kiasi gani cha data unataka kutumia kwa siku pia ita kuonyesha matumizi ya data kwa siku, wiki pamoja na mwezi huku iki-onyesha ni app gani inayotumia data zaidi.

6. 2018 FIFA World Cup Russia™ Official App

The Official FIFA App

Zimebaki siku 6 tu, na kama jina linavyo jieleza app hii itakusaidia kuweza kupata habari zote kuhusu kombe la duniani na pia app hii itakupa uwezo wa kuchagua timu unayo ipenda ili kupata habari zaidi za timu hiyo, pia itakusaidia kupata ratiba ya makundi, matokeo, historia ya timu pamoja na mambo mengine mbalimbali. Ukweli ni kuwa inawezekana uziweze kuangalia mechi zote kupitia TV yako, lakini kwa kupitia app hii utakuwa na uwezo wa kupata habari zote kuhusu yote yanayojiri kwenye kombe la dunia.

Na hizo ndio app nzuri nilizo kuandalia kwa siku ya leo, Kama ulipitwa na makala iliyopita ya app nzuri za android unaweza kusoma na kujaribu app hizo hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia usisahau kupakua app ya Tanzania Tech kwa habari za haraka za Teknolojia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use