Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy A6 (2018)

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hizi hapa sifa na bei za Galaxy A6 na A6 Plus
Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy A6 (2018) Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy A6 (2018)

Baada ya tetesi na kuvuja kwa picha mbalimbali za simu mpya za Samsung Galaxy A6 pamoja na Galaxy A6 Plus (2018), Hatimaye kampuni ya Samsung imetangaza kuzindua rasmi simu hizo siku ya leo. Mbali na muonekano wake unaofanana na Galaxy S9, simu hizi zinakuja na maboresho mengi sana ikiwa pamoja na teknolojia ya sauti ya Dolby Atmos, Bixby Vision, Bixby Home, Bixby Reminder, pamoja na huduma ya malipo ya Samsung Pay.

Mbali ya kuja na maboresho hayo, Galaxy A6  inakuja na kioo cha inch 5.6 chenye teknolojia ya Super AMOLED Infinity Display ambacho kinayo Aspect ratio ya 18.5:9 aspect ratio, pamoja na sifa nyingine kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A6 (2018)

Advertisement

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.6 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, 18.5:9 ratio (~294 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53, Exynos 7870 Octa Chipest.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T830 MP1
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 32 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 3 na nyingine itakuwa na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye (f/1.7), phase detection autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.9) pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold, Blue na Lavender
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by)
    , inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Sifa za Samsung Galaxy A6 Plus (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, 18.5:9 ratio (~411 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450
    Chipest.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 32 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 3 na nyingine itakuwa na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/1.9), phase detection autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ikiwa na Megapixel 16 (f/1.7) na nyingine ikiwa na Megapixel 5 (f/1.9) zote zikiwa na phase detection autofocus na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold, Blue na Lavender
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by)
    , inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Simu zote hizi mbili zitaanza kupatikana rasmi mapema mwezi huu na zita anza kupatikana kwa nchi za Ulaya, Asia, na Amerika ya Kusini na baadae zitapatina kwenye nchi za Afrika, Korea ya kusini pamoja na China.

Kwa upande wa bei Galax A6 (2018) Itapatikana kwa dollar za marekani $410 sawa Tsh 937,000 na upande wa Galaxy A6 Plus (2018) yenyewe itakuwa inauzwa kwa dollar za marekani $480 sawa na makadirio ya Tsh 1,100,000. Kumbuka bei hizi ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivyo bei inaweza kuongezeka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use