Samsung Galaxy J2 Pro Simu Janja Isiyokuwa na Internet

Maalum kwaajili ya wanafunzi na aina namna yoyote ya kuwezesha Internet
Samsung Galaxy J2 Pro isiyo na Internet Samsung Galaxy J2 Pro isiyo na Internet

Huwenda ukawa unajiuliza, inakuaje simu janja alafu haina internet.? Basi ngoja nikujuze kidogo, nchini korea ya kusini ambapo ndio makao makuu ya Samsung yalipo wanafunzi wa nchini humo huwa na aina moja ya mtihani unaoitwa Suneung aina hii ya mtihani sio sawa na aina nyingine za mitihani inayofanywa na wanafunzi kawaida duniani kote.

Bali Suneung ni moja kati ya mitihani inayo tambulika kuwa ni mitihani inayo tathimini maisha ya mwanafunzi kwa ujumla kwa kupima uwezo wa mwanafunzi, mitihani hii inasemekana kutabiri ni chuo gani mwanafunzi ataingia ikiwa pamoja na maisha ya mwanafunzi kwa ujumla. Siku ya mtihani nchi nzima ya korea ya kusini utambua uwepo wa mtihani huu na baadhi ya mambo kama usafiri wa anga husutishwa pamoja na usafiri wa mabasi barabarani kuongezwa kwaajili ya kuhakikisha wanafunzi hawachelewi mtihani huo.

Mbali na hayo wakati mwingine polisi hutumika kuwasindikiza wanafunzi wanapo enda kwenye mtihani huo ili kuhakikisha wanafika salama, Vilevile kuonyesha umuhimu wa mtihani huo, wazazi pamoja na wanafunzi wengine ambao hawafanyi mtihani huo ukusanyika kwenye eneo la mtihani ili kufanya wanafunzi wajisikie vizuri na kuwapa ujasiri wakati wa mtihani. Mtihani huu hufanyika kila mwaka mwezi November.

Advertisement

Sasa kuonyesha umuhimu wa siku hii, Kampuni ya Samsung imezindua simu hiyo ya Samsung Galaxy J2 Pro ambayo itakuwa ni kwaajili ya wanafunzi nchini humo. Kama nilivyosema awali simu hiyo haina Internet wala haina Wi-Fi kifupi ni kwamba simu hiyo haina namna yoyote ya kuganishwa na internet na hii ni kwa sababu Samsung ina amini kuwa simu hizo zitakuwa msaada kuzuia wanafunzi kupoteza umakini pale siku ya mtihani huo inapofika.

Mambo mengine kwenye simu hii yanafanya kazi kama kawaida, unaweza kutuma meseji, unaweza kupiga simu ikiwa pamoja na kupiga picha. Simu hiyo pia inakuja na sifa nyingine nzuri tu kama vile, Kioo cha inch 5 chenye teknolojia ya QHD AMOLED, Processor ya Galaxy J2 Pro inakuja ikiwa na uwezo wa 1.4GHz quad-core inayo saidiwa na RAM ya GB 1.5. Vilevile simu hiyo inakuja na Battery yenye uwezo wa 2,600mAh. Simu hii inakuja na sehemu ya kuweka Memory Card na kamera ya Megapixel 8 kwa nyuma na Megapixel 5 kwa mbele.

Simu hii inauzwa nchini korea ya kusini pekee na bado haijulikani kama simu hii inaweza kuja na nchi nyingine. Wanafunzi wa nchini humo wanaweza kuipata kwa Won 200,000 sawa na Tsh 425,000 kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.

Kwa sasa Samsung wanafanya promosheni kwaajili ya wanafunzi nchini humo watakao fanya mtihani huo mwaka ujao na mara baada ya kumaliza mtihani huo wanafunzi wataweza kubadilisha simu hiyo na kuchukua simu za Samsung kati ya simu za Galaxy S, Galaxy Note au Galaxy A-series.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use