in

Twitter Kuja na Sehemu Mpya ya Video Inayofanana na Snapchat

Sehemu hii inategemewa kuja kurahisisha jinsi ya kupost video

Twitter Video

Hivi leo mtandao maarufu wa biashara wa Bloomberg, umetoa ripoti mpya inayodai kuwa Twitter ipo kwenye hatua za awali za kutengeneza sehemu mpya ya mtandao huo ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya Video.

Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo yaliyopo kwenye mtandao huo, sehemu hiyo inategemewa kufanana na baadhi ya sehemu kwenye mtandao wa Snapchat. Kwa mujibu wa maelezo hayo Twitter tayari inayo muundo maalum uliokamilika kwa ajili ya sehemu hiyo lakini muundo huo unategemewa kuendelea kuboreshwa zaidi.

Twitter haijatoa tamko lolote juu ya kuja kwa sehemu hiyo na bado hakuna uhakika kama sehemu hiyo itakuja siku za karibuni. Wataalamu wa mambo ya mtandao wanasema kuwa lengo la sehemu hiyo mpya ni kupunguza hatua za kufuata wakati mtu anataka kutuma video kwenye mtandao wa Twitter.

Kwa sasa hakuna tamko lolote kuhusu sehemu hiyo kutoka kwa uongozi wa mtandao huo huku wafanyakazi wake pia wakikataa kusema lolote kuhusu ukweli wa ujio wa sehemu hiyo. Tunaendelea kufuatilia habari hii na tuta kuhabarisha pale tutakapo pata mwendelezo wa taarifa hii.

Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.