in

Vivo V7+ Simu ya Kwanza Yenye Kamera ya Mbele ya MegaPixel 24

Hii ndio simu yenye kamera kubwa ya selfy kuliko zote

Tumesha fikia robo tatu ya mwaka 2017, bado kampuni mbalimbali zinaendelea kutoa simu mbalimbali na zenye kutumia teknolojia ya kisasa. Lakini pamoja na yote hayo hatujafaikiwa mpaka sasa kusikia simu yenye uwezo wa megapixel 24 kwa kamera ya mbele.

Kampuni ya Vivo ambayo ndio watengenezaji wa simu za Vivo ambazo zinatumika sana barani Asia na ulaya hivi karibuni imetoa simu yake mpya ya Vivo V7+ ambayo inakuja na uwezo wa kipekee wa kamera ya mbele ya Megapixel 24 na huku ikiwa na Megapixel 16 kwa kamera ya nyuma.

Sifa zingine za simu hii ni kama vile Processor ya 1.8GHz octa-core Qualcomm Snapdragon 450 processor clubbed yenye Adreno 506 GPU. RAM ikiwa ni GB 4 pamoja na ukubwa wandani wa GB 64 huku ikiwa na uwezo wa kupokea memory card ya hadi GB 256.

Kwa upande wa kioo simu hiyo ina kioo cha inch 6 chenye uwezo wa 720p IPS LCD ikiwa na resolution ya 1440×720 pixel, kwa mfumo wa uendeshaji simu hii inatumia mfumo wa Android 7.1.2-huku ikiwa na mfumo wa maboresho wa OS 3.2 Vivo’s custom ROM, kwa upande wa battery Simu hii inatumia battery yenye uwezo wa 3,225mAh.

Kampuni ya Apple Yazindua Simu Mpya ya iPhone SE (2020)

Simu hii imetoka rasmi huko nchini india na inategemewa kuingia sokoni hivi karibuni lakini bado haijajulikana kama toleo hilo litatoka kwa dunia nzima itakubidi kusubiri ili uweze kujua kuhusu hilo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : India Today

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.