in

Mambo Muhimu Kujua Kuhusu Mtandao wa YouTube

Haya ni baadhi ya mambo ambayo ni vizuri ukajua kuhusu Youtube

Mambo Muhimu Kujua Kuhusu Mtandao wa YouTube

Youtube ni moja kati ya mtandao mkubwa sana wa video, lakini pia youtube ni moja kati ya sehemu kubwa sana ya kutafuta vitu yaani kwa maneno mengine ni kuwa baada ya Google, Youtube ni sehemu nyingine ambayo hutumika zaidi kutafuta vitu mtandaoni.

Lakini leo hatuta angalia hayo bali natakanikujuze mambo haya muhimu ambayo kwa namna moja au nyingine ni muhimu wewe kujua, basi twende moja kwa moja….

  • Youtube Ilianzishwa Sababu ya Paypal

Mtandao wa Youtube uligunduliwa mwaka 2005 na Chad Hurley, Steve Chen, pamoja na Jawed Karim, watatu hawa walikuwa wanajuana kwa kuwa walikua wanafanya kazi sehemu moja yaani kwenye kampuni ya Paypal ambayo ni kampuni inayo jihusisha na mambo ya malipo kupitia mtandaoni. Hivyo kama sio watatu hawa kujuana kupitia kampuni hiyo labda leo mtandao wa Youtube usinge kuwepo.

  • Video ya Kwanza Kuwekwa kwenye Mtandao wa Youtube

Video ya kwanza kabisa kuwekwa kwenye mtandao wa youtube iliwekwa na mmoja wa watumiaji wa mwanzo wa mtandao huo Yakov Lapitsky, Video hiyo ilikuwa ikionyesha mmoja wa wagunduzi wa mtandao huo Jawed Karim akizungumzia kuhusu tembo video hiyo iliwekwa tarehe Apr 23, 2005. Unaweza kuangalia video hiyo hapo chini.

Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19

  • Mtandao wa Youtube Umezuiwa Kwenye Nchi Hizi

Kama wewe ni mmoja wa watuambao wanafaidi mtandao wa youtube kwa kujifunza mambo mbalimbali basi kumbuka kutumia vizuri mtandao huo kwani kwenye baadhi ya nchi serekali imekataza kutumika kwa mtandao huo kwa wakati mmoja au mwingine. baadhi ya nchi hizo ni China, Syria, Bangladesh, Iran, Pakistan, Sudan, Tajikistan, Turkmenistan. Baadhi ya nchi hizi kwa sasa zina ruhusu mtandao huo kutokana na kubadilisha sheria zao.

  • Unaweza Kujaribu Sehemu Mpya za Youtube Kabla Hazijatoka

Kwa wale wanao tembelea mtandao wa Tanzania Tech basi hili sio jipya sana kwani tayari tulisha angalia jinsi ya kufanya hivyo, kama unataka kuangalia sehemu mpya kwenye mtandao wa youtube ni lazima uwe na kompyuta kisha bofya link hii www.youtube.com/new kisha bofya kitufe cha Try it Now kwa maelezo zaidi soma hapa.

  • Video Ndefu Kuliko Zote Ina Muda wa Masaa 571

Video ambayo ina urefu kuliko video zote kwenye mtandao wa youtube ilikuwa na masaa 571, Dakika 1 na sekunde 41. Video hii ambayo sasa imeondolewa kwenye youtube ilikuwa inachukua muda wa siku 23 kuweza kuangalia video yote kupitia mtandao huo.

  • Tafuta “Do the Harlem shake” Kwenye Youtube Uone Maajabu
Chaja yenye Uwezo wa Kujaza Simu 100% Ndani ya DK 19

Kama uko karibu na kompyuta basi ingia kwenye mtandao wa Youtube kisha andika maneno haya “Do the Harlem shake” kwenye kisanduku cha kutafuta kisha bofya tafuta kisha utaona ukurasa mzima wa youtube ukicheza staili hiyo ya Harlem shake… Jaribu sasa uone maajabu, haina madhara yoyote.

Na hayo ndio baadhi tu ya mambo ambayo nimeku andalia kwa leo, usiache kujiunga nasi jumapili ijayo kujifunza maengine mengi ya kujua kuhusu teknolojia. Kama una maoni au unalo la kuongezea kwenye mambo haya, basi unaweza kutuandikia hapo china nasi tutaongeza kwenye makala hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Factslides, Mashable, LEMMiNO

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 3

Toa Maoni Hapa
  1. Naomba kuulza,hv Channel za YouTube Zinatofautianaje?
    Zipo kwa ajiri ya business na ambazo sio,au zote ni kwa ajiri ya business?

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.