in

Agundua Kompyuta Yenye Kujua Harufu ya Kansa na Mabomu

Raia wa Nigeria Oshi Agabi agundua kompyuta yenye kujua harufu

Raia mmoja wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazo tumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini hapa Tanzania. Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya mabomu na unaweza kutumiwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, alisema.

Vilevile kifaa hicho kilicho na ukubwa wa modem na kupewa jina Koniku Kore kinaweza kuwa ubongo wa roboti za siku za usoni. Kampuni kubwa za kiteknolojia, ikiwemo Google hadi Micrososft ziko katika harakati ya kutengeza roboti inayoweza kuwa na akili ya mwanadamu, hivyo inawezekana jamaa huyu kupata nafasi kupitia kampuni hizo.

Bwana Agabi alizindua kifaa hicho cha koniku yapata mwaka mmoja uliopita na amefanikiwa kuchangisha dola milioni moja kama ufadhili na anasema kuwa kifaa hicho kimempatia dola milioni 10 katika mikataba na kampuni za usalama.

Koniku Kore ni kifaa kilichotengezwa kwa kutumia neva na silicon ambacho kina sensa zinazoweza kutambua harufu. ”Unaweza kuzipa neva hizo maelezo ya ni nini unachotaka zifanye ambapo upande wetu tunaziambia kutoa seli zinazoweza kutambua harufu”,alisema.

Video : Teknolojia Mpya Ambazo Huwenda Ulikuwa Huzijui

Kungamano la TEDGlobal limeanza toka tarehe 27 mwezi huu huko Arusha, Tanzania na linategemewa kumalizika tarehe 30 mwezi huu. Kungamano hilo lina lengo la kushirikishana mawazo mbalimbali pamoja na utatuzi wa matatizo hayo yanayo zunguka jamii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : CNN

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.