in

LG Kuja na LG Q6 Simu Mpya ya Kisasa Yenye Kioo cha FullVision

Kama umeshindwa kuimudu LG G6 Basi usiwe na wasiwasi..

Baada ya kampuni ya LG kutoa simu mpya ya LG G6, simu ambayo inakuja na teknolojia bora pamoja na uwezo mkubwa kwenye kioo chake cha kisasa cha inch 18:9, lakini inawezekana simu hii ikiwa ni bei ghali sana kwako kutokana na kuuzwa kwa Rupee za india  Rs. 37,990 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,318,676.00.

Kama simu hiyo ni ghali kwako basi usijali kwani kampuni ya LG imeleta simu mpya ya LG Q6 ambayo inakuja na teknolojia ya kioo sawa na simu ya LG G6, simu hii inakuja na uwezo mkubwa lakini kwa bei ya kawaida pamoja na teknolojia nzuri na bora kama ile ya FullVision ambayo inafanya simu ya LG Q6 kuwa na kioo kikubwa kisicho na ukingo.

Simu hii ya LG Q6 inakuja kwa aina tatu yaani LG Q6+ yenye uwezo wa ram ya 4GB na ukubwa wa ndani wa GB 64 na LG Q6 yenye uwezo wa ram ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32 pamoja na LG Q6α yenye ram ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16. Simu zote hizi zinakuja na processor ya Snapdragon 435 chip na kioo chenye ukubwa wa inch-5.5 sawa na 2,160 x 1,080.

Simu hizi pia zimetengenezwa kwa kava la aluminum huku zikiwa na uwezo wa facial recognition pamoja na kamera bora yenye uwezo wa kuchukua nyuzi 100-degree wide, simu hizi za LG Q6 zitakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 5 pamoja na ya nyuma ya Megapixel 13 huku zote zikiwa na battery zenye uwezo wa 3,000mAh. Simu hizi zitanza kuuzwa rasmi mwezi ujao huko nchini Asia kabla ya kutoka kwa dunia nzima.

Kampuni ya TECNO yazindua CAMON 15 Hapa Tanzania

Kwa ufupi hizi hapa ndio sifa za simu hizo, bado kwa sasa haijajulikana bei za simu hizo lakini simu hizo zitatofautiana bei kutokana na ukubwa wa ndani wa simu hizo.

 • Chipset: Qualcomm® Snapdragon™ 435 Mobile Platform
 • Display: 5.5-inch 18:9 FHD+ FullVision Display (2160 x 1080 / 442ppi)
 • Memory: Q6+: 4GB RAM / 64GB ROM, Q6: 3GB RAM / 32GB ROM, Q6α: 2GB RAM / 16GB ROM
 • Camera: Rear 13MP Standard Angle / Front 5MP Wide Angle
 • Battery: 3,000mAh (embedded)
 • Operating System: Android 7.1.1 Nougat
 • Size: 142.5 x 69.3 x 8.1mm
 • Weight: 149g
 • Network: LTE / 3G / 2G
 • Connectivity: Wi-Fi 802.11 b, g, n / Bluetooth 4.2 / NFC / USB Type-B 2.0
 • Colors: LG Q6+: Astro Black / Ice Platinum / Marine Blue, LG Q6: Astro Black / Ice Platinum / Mystic White / Terra Gold, LG Q6α: Astro Black / Ice Platinum / Terra Gold
 • Other: Face Recognition / Google Assistant / Square Camera / Steady Record / FM Radio

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.