in

Sasa Programu ya Kaspersky ni Bure Kabisa (Download Hapa)

Utaweza kutumia programu ya Anti Virus ya Kaspersky ya bure kabisa

Kwa namna moja ama nyingine wote tunaijua programu ya Kaspersky na kama bado huifahamu basi programu hii ni moja kati ya programu bora sana ya kulinda simu au kompyuta yako ili athiriwe na programu mbaya pamoja na Virusi vya aina mbalimbali vinavyo patikana mtandaoni.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali programu hii pia ni moja kati ya programu bora sana kwa kufanya kazi ya kuondoa virus na imeshinda tuzo nyingi mbalimbali kama programu bora ya Anti Virus kwa miaka iliyopita.

Katika kuonyesha ubora wake kampuni ya Kaspersky Lab ambayo ndio watengenezaji wa programu hiyo sasa wanakupa uwezo wa kutumia programu ya Kaspersky bure kabisa, bila kulipia kama huna uwezo huo. Programu hiyo ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa kuuzwa pekee kwa dollar za marekani $50 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 111,900.

Kwa sasa utaweza kupata programu hiyo bure kabisa na utaweza kutumia programu hiyo kwa mwaka mzima bila kulipia chochote, aitha kampuni hiyo imeleta toleo hilo jipya la Kaspersky la bure lakini toleo la kulipia bado litakuwa pale pale na utapewa uwezo wa kuchagua kununua au kutumia toleo la bure ambalo lina vitu vichache kuliko lile toleo la kulipia.

Fahamu Njia Rahisi ya Kujua Mapato na Matumizi Yako

Kwa sasa unaweza kudownload programu ya Kaspersky ya bure kwaajili ya kompyuta yako kupitia kitufe hapo chini, bofya hapo kisha chagua Download Now kupitia tovuti ya Kaspersky.

Download Kaspersky Bure Hapa

Programu hii ya bure kwa sasa ni kwaajili ya kompyuta pekee, kama unataka kupata programu ya Kaspersky kwaajili ya smartphone yako unaweza kudownload kupitia soko lako la Play Store kwa watumiaji wa Android au App Store kwa watumiaji wa iOS.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Engadget

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 2

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.