Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mozila Yaleta Kisakuzi Kipya cha Binafsi cha Firefox Focus

Kama unataka kutumia kisakuzi cha binafsi cha Kwenye simu yako
Firefox focus Firefox focus

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawapendi kuo onyesha historia ya vitu ulivyopitia mtandaoni kwenye simu yako, basii hii ni maalum kwaajili yako.

Hivi karibuni kampuni ya Mozila imetangaza aina mpya kabisa ya kisakuzi ambacho kazi yake kubwa ni kuzuia mtu kujua ulichotafuta kwenye mtandao ni nini, kwa mara ya kwanza kisakuzi hichi kilitambulishwa kwenye mfumo wa iOS na kuonekana ni muhimu sana na kutokana na maombi ya watu wengi sasa kisakuzi hicho kimekuja rasmi kwenye Android.

Advertisement

Umuhimu wa kisakuzi hichi utaweza kuzima matangazo yote ya kurasa unazotembelea kwa kuwasha sehemu maalumu ya trackers blockers ambayo inapatikana kwenye sehemu ya settings kwenye kisakuzi hicho. Kingine ni kuwa kisakuzi hichi kinafuta kila kitu ulichotembelea pale tu utakapo funga kisakuzi hicho.

Unaweza kupakua programu hii mpya ya Android kwa kutumia link hiyo hapo chini nauhakika utaipenda programu hiyo kwa jinsi inavyofanya kazi. Lakini pia kama bado huja download programu hii kwa mfumo wa iOS basi unaweza pia uka download hapo chini.

Download FireFox Focus kwa Mfumo wa Android

Download FireFox Focus kwa Mfumo wa iOS

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use