Microsoft Yaja na Keyboard Mpya Yenye Sehemu ya FingerPrint

Microsoft yaja na aina mpya ya Keyboard mpya bomba sana
Microsoft Keyboard Microsoft Keyboard

Kampuni ya Microsoft inaendelea kuwa kampuni bora sana kadri siku zinavyo kwenda, kuthibitisha hilo hivi karibuni kampuni ya microsoft imeleta keyboard yake mpya bora yenye sehemu ya fingerprint, hivyo sasa huna haja ya kuingiza password kufungua kompyuta yako bali sasa tumia fingerprint hata kama kompyuta yako haina uwezo huo.

https://www.youtube.com/watch?v=YDpGtDzAw4I

Keyboard hiyo iliyotengenezwa kwa Aluminium inakuja na ubora wa hali ya juu huku ikiwa na vibonyezo zinavyo fanana na vile vya keyboard za kompyuta za Apple. Zaidi keyboard hii inaweza kutumika na kompyuta yoyote yenye bluetooth pamoja na uwezo wa mfumo wa Windows 8 pamoja na Windows 10, kuhusu chaji keyboard hii inatumia battery ndogo za AAA ambazo kwa mujibu wa microsoft ukiwa na battery bora unaweza kutumia keyboard hiyo kwa muda wa miezi miwili au zaidi.

Advertisement

Kwa upande wa bei, keyboard hiyo inauzwa kwa dollar za marekani $130 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 290,940.00 bila kodi na mouse ya keyboard hiyo itauzwa kwa dollar za marekani $50 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 111,900.00 bila kodi. Kumbuka viwango vyote vya pesa ni kutokana na viwango vya kubadilisha pesa vya siku ya leo 19-06-2017.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use