Ethiopia Inayo Mashine Kama ATM za Kuweka Filamu Kwenye Flash

Ulimwengu mpya wa filamu za wizi unapatikana ethiopia na kwa teknolojia mpya
Filamu Filamu

Huko nchini Ethiopia sasa kuna aina mpya ya teknolojia ambayo inakupa uwezo wa tofauti wa kupata filamu kwa haraka na bila kutumia gharama kubwa. Teknolojia hiyo ambayo imeonekana kwenye sehemu mbalimbali za miji ya ethiopia inabadilisha mawazo yako kabisa kuhusu uwezo wa upatikanaji wa movie au filamu za wizi (pirate movies) duniani kote.

Teknolojia hiyo ambayo ni mashine ya mfano wa ATM inakupa uwezo wa kupachika USB Flash na kuchagua movie au filamu unayotaka kwenye kioo cha mashine hiyo na kuituma moja kwa moja kwenye USB flash yako. Kifaa hicho kilichopewa jina la SwiftMedia kiosks kinaendeshwa na kampuni ya Escape Computing ambayo inauza filamu hizo kwa bando la gharama ya pesa za ethiopia kati ya 25 birr, 50 birr na 100 birr sawa na shilingi za kitanzania 2500, 5000 na 10,000.

[envira-gallery id=”10557″]

Mashine hiyo haitaji mtu ili iweze kufanya kazi kwani kila kitu ni moja kwa moja yani Automatic, hata hivyo bado haijajulikana kama unalipia pesa kwenye mashine hiyo au lah! lakini.. pamoja na yote hii ni aina mpya ya teknolojia na aina mpya ya wizi wa filamu ambao nadhani ukibadilishwa na kutumia vizuri unaweza kubadilisha kabisa soko la filamu kwa hapa kwetu Tanzania ukizingatia DVD na CD zimesha pitwa na wakati..Ni maoni yangu tu!

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use