Jinsi ya Kuanzisha Darasa la Mtandaoni na Kualika Wanafunzi

Kama unataka kuwa mwalimu au kujifunza kupitia madarasa mtandaoni
Darasa Mtandaoni Darasa Mtandaoni

Teknolojia inaendelea kukua kila siku na hata njia ambazo wote tunajifunza zimekua tofauti kidogo, Teknolojia imetufungulia dunia kwa kuwezesha urahisi wa kujifunza mambo kwa undani kupitia vifaa kama simu za mkononi, kompyuta na vifaa vingine kama hivyo. Watoa elimu nao (walimu) sasa wame wekewa urahisi zaidi kwa wa kutoa elimu kwa haraka na urahisi moja kwa moja kupitia mtandao, kupitia hili leo Tanzania Tech tunaenda kukuonyesha namna bora ya kuanzisha darasa la mtandaoni pamoja na kualika wanafunzi.

Njia hii inaweza kutumiwa na walimu wa shule zote msingi, sekondari, vyuoni na hata walimu wa kawaida wanaofundisha kitu chochote kile kupitia mtandaoni kifupi ni kwamba njia hii ni bora sana na inakupa platform yenye ubora wa hali ya juu kufanya kile unachotaka katika swala zima la kutoa elimu, baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tukangalie somo hili la leo.

Advertisement

Kwa kuanza unaitaji kuwa na akaunti ya mtandao wa Google pia hakikisha unakuwa na email (barua pepe) ya mtandao huo yaani Gmail kama huna barua pepe ya Gmail unaweza kujisajili kupitia hapa, huduma hii inatolewa na Google na imefunguliwa hivi karibuni hivyo twende tukajifunze wote mara ya kwanza jinsi ya kuitumia. Baada ya kuhakikisha una yote hayo hapo juu endelea kwenye hatua ya pili kwa kutembelea ukurasa huu wa Google Classroom.

Hapo utapelekwa kwenye ukurasa maalum ambao unatakiwa kuthibitisha akaunti yako ambayo unataka kutumia kisha maliza kwa kubofya Continue baada ya hapo sasa utakuwa uko tayari kujiunga na mtandao bora wa Google Classroom ili kujifunza au kutoa elimu mtandaoni. Ili Kuanza kutumia bofya alama ya jumlisha iliyoko upande wa juu kulia kisha kama wewe ni mwalimu na unataka kutengeneza darasa basi bofya Create Class kama wewe ni mwanafunzi basi bofya Join Class na utaletewa sehemu ya kuingiza code ambazo utakuwa umepewa na mwalimu wako. Kujifunza jinsi ya kutumia platform hii kama mwanafunzi au mwalimu angalia video hapo juu.

Kama utakuwa kuna mahali umekwama au una swali au unaitaji maelekezo ya aina yoyote usisite kutandikia maoni yako hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja. pia unaweza kujiunga na darasa lete la mtandaoni kwa kutumia code hizi anika bila mabano (dhwz7v) hakikisha unaziandika kwenye fomu inayopatikana juu baada ya kubofya kitufe cha (Join Class).

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use