Facebook Yaja na “Facebook M” Kwaajili ya Facebook Messenger

Facebook sasa yaleta Artificial Intelligence au AI kwaajili ya Facebook Messenger
Facebook M Facebook M

Hivi karibuni Facebook imetangaza sehemu mpya kwaajili ya Facebook Messenger inayoitwa Facebook M, sehemu hii itakusaidia kupata mapendekezo kadhaa wakati unachat na ndugu, jamaa au rafiki kupitia programu za Facebook Messenger.

Facebook M kwa sasa inapatikana kwenye nchi za marekani  huku ikiwa inatoa uwezo wa kufanya shuhuli mbalimbali kama vile, pale unapokuwa unachat na mtu na mkapanga kukutana kwaajili ya chakula cha mchana basi Facebook M itatoa mapendekezo ya migahawa au hoteli nzuri ambazo zitafaa kwaajili ya kikao chenu, vilevile Facebook M inauwezo wa kukupa mapendekezo ya usafiri ikiwa pamoja na kutoa mapendekezo ya njia salama na rahisi za kutuma pesa (sehemu ambayo ipo kwa nchi za marekani pekee).

Facebook M inatumia mfumo maalaum wa kuangalia chat zako na watu wako ili kukupa mapendekezo hayo, mfumo huu ambao ni waki roboti (AI / Artificial Intelligence) unategemewa kusambaa kwa dunia nzima hivi karibuni kupitia programu za Facebook Messenger za Android pamoja na iOS .

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use