Viber Kuongeza Sehemu Mpya ya Meseji Zinazojifuta Zenyewe

Viber yaongeza sehemu mpya kwa watumiaji wake milioni 800
Viber Viber

Unaweza ukawa huijui au hujawahi kujaribu kutumia programu ya Viber, hii ni programu ya kuchat kama ilivyo WhatsApp ambayo kwa sasa ina watumiaji takriban milioni 800 duniani kote. Programu hii inaongoza sana kutumika kwa nchi za Asia, Eastern Europe pamoja na Northern Africa.

Sasa katika kuhakikisha watumiaji wake wote wanapata kutumia programu hiyo kwa raha na kwa usalama programu hiyo inakuja na sehemu mpya inayoitwa “secret chat”. Sehemu hii itakuwezesha kutumia programu hiyo uku vitu unavyo chat vikiwa na uwezo wa kufutika ndani ya muda maalum (self destruct), sehemu hiyo inakuja baada ya kampuni hiyo kuleta sehemu mpya ya kukuwezesha kuweka password kwenye meseji zako ambazo unachat.

Viber kwa sasa inajitahidi kuongeza sehemu mpya ili kuweza kuvutia watumiaji wengi kutumia programu hiyo ambayo iko kwenye mfumo wa Android pamoja na iOS, unaweza kupakua programu hiyo sasa uweze kujaribu kupitia Play Store pamoja na App Store.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia kuwa wakwanza kudownload App ya Tanzania Tech kutpitia Play Store au unaweza kujiunga nasi kupitia Channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use