Windows 10 Yaja na Game Mode na Hivi Ndivyo Inavyofanya Kazi

Jiandae kwaajili ya game mode kwenye kompyuta yako yenye windows 10
Windows Game Mode Windows Game Mode

Microsoft kupitia Windows 10 hivi karibuni inatarajiwa kuja na sehemu mpya ya Game Mode, sehemu hii mpya itakusaidia kuongeza nguvu ili kufanya kompyuta yako yenye Windows 10 kuweza kucheza game vizuri na kwa urahisi zaidi.

Wakati tukiwa tunasubiria sehemu hiyo inayotarajiwa kuja na toleo jipya la Windows 10, Microsoft imeanza kuelezea jinsi sehemu hiyo mpya itakavyofanya kazi. Akielezea mmoja wa waatamu kutoka Microsoft alisema kuwa, pale Game Mode inapowashwa kwenye kompyuta yako nguvu zote zinaelekezwa kwenye CPU pamoja na GPU ambavyo huongeza frame rate ili kufanya uweze kucheza game vizuri na kwa urahisi.

Advertisement

Vilevile Microsoft imeweka game maalum kwaajili ya sehemu hiyo ambayo utaweza kuiwasha ukiwa unacheza game kwa kubofya “Windows + G”. Game Mode, Game Bar, pamoja na gaming options zilizopo kwenye settings zote zitaanza kupatikana kwenye toleo jipya la Windows 10 linakuja kama Windows 10 Creators Update, linalotarajiwa kutoka mwaka huu 2017.

Kwa Habari zaidi za lini Toleo hili litafika hapa Tanzania na jinsi ya kudownload toleo litakapo toka, endelea kutembelea Tanzania Tech au Download App ya Tanzania Tech ili kupata habari pindi zitakapo toka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use