Facebook Nayo Kuleta Sehemu Mpya ya Facebook Stories

Jiandae kwaajili ya sehemu hii mpya kutoka facebook
facebook storiesz facebook storiesz

Kwa muda sasa Facebook imekua ikifanya majaribio ya sehemu mpya ya Facebook Stories kwenye programu zake za Facebook Messenger za mifumo ya iOS pamoja na Android. Majaribio hayo yaliokua yakifanyika kwa watumiaji wa nchini Poland, sasa yameamia nchini Ireland hii ikiwa ni hatua za karibu za kuanza kusambaza kwa sehemu hiyo kwa watumiaji wote duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Business Insider ya nchini marekani sehemu hiyo mpya itakuwa sawa na ile ya kwenye programu za Snapchat pamoja na Instagram. Kwa kutumia sehemu hiyo Stories zote zitatokea kwa juu kama vile kwenye programu ya instagram inavyokua, pia mtumiaji wa sehemu hiyo atawezeshwa kutuma storie yake ambayo haita onyeshwa kwenye sehemu ya timeline bali stories zote zitakuwa zikionekana kwenye sehemu hiyo maalum ya Facebook Stories.

Mpaka sasa bado haijajulikana tarehe halisi ya lini sehemu hiyo itanza kutoka kwenye programu zote za Facebook Messenger za iOS pamoja na Android, lakini dalili zinaonyesha watumiaji wa Facebook watapata sehemu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

Advertisement

Kujua zaidi kuhusu sehemu hii enendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku ili uwe wakwanza kufahamu habari zote za teknolojia au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka pia kwa kupitia channel yetu ya Youtube ya Tanzania Tech utaweza kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia hivyo jiunge nasi leo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use