Youtube Star Alipotolewa Kwenye Ndege Baada ya Kuongea Kiarabu

Mtumiaji maarufu wa mtandao wa youtube Adam Saleh alipotolewa kwenye ndege baada ya kuongea kiarabu
Youtube Star Youtube Star

Star muigizaji na mtumiaji maarufu wa mtandao wa youtube Adam Saleh na rafiki yake jana wameshushwa kwenye ndege baada ya kuongea kiharabu, Star huyo mwenye watu zaidi ya milioni mbili kwenye youtube alionyesha tukio lilivyokuwa wakati wakiwa wanashushwa kwenye ndege hiyo ya kampuni ya Delta ya nchini marekani.

Katika tweet ya star huyo  Adam Saleh alionyesha akiwa na hasira sana wakati wakiwa wanashushwa kwenye ndege hiyo na watumishi wa ndege hiyo. Tweet hiyo imeleta majadiliano makubwa kwenye mitandao ya kijamii na baadae kupelekea kuleta hash tag mpya ambayo imekua maarufu ya #BoycottDelta.

Kwa sasa kampuni hiyo ya ndege ya Delta inasema inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ina sisitiza kuwa haipendi ubaguzi wa rangi hivyo ni lazima itashulikia swala hilo, Hata hivyo leo asubuhi hii Adam Saleh pamoja na rafiki yake huyo baadae wameweka video wakiwa wanasimulia tukio zima jinsi lilivyo tokea.

Bado sakata hilo linaendelea na bado watu mbalimbali wanaonekana kutoa mawazo yao kuhusu tukio hilo zima, je wewe unasemaje kuhusu hili unaweza kutoa maoni yako hapo chini. Ili kuendelea kujua kuhusu tukio hili zima endelea kupitia post hii kila siku ili kujua hatua zilizochukuliwa baada ya tukio hilo.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use