Instagram Kuleta Uwezo wa Kuzima Maoni Kwenye Picha

Sasa programu ya Instagramu inakuja na uwezo wa kumuwezesha mtumiaji kuzima comment kwenye picha
Instagram Instagram

Hivi karibuni programu ya Instagram inategemewa kuongezewa baadhi ya sehemu mpya ambazo zimekua zikiombwa na kungojewa na watu wengi sana, katika kutimiza maombi ya watumiaji wake Instagram imetangaza kuleta sehemu mpya ambayo itakuwezesha kuzima (Maoni) comment kwenye picha zako.

Sehemu hiyo mpya itapatikana kwa kubofya “Advanced Settings” kabla ya kuposti picha na kisha “Turn Off Commenting” vilevile sehemu hiyo itaweza kuonekana baada ya kupost picha yako ili kusaidia kuwasha tena comment kama utahitaji.

Toleo hilo jipya linakuja sambamba na sehemu nyingine mpya ya ku-kuwezesha kulike comment ya mtu kwa kubofya kitufe cha kupenda (like) kilichoko mbele ya comment ya mtu. Sehemu zote hizo zinategemewa kuja kwenye matoleo yake yanayokuja hivi karibuni hivyo hakikisha una update programu hiyo mara kwa mara.

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use