Samsung Kuleta Toleo Jipya la Galaxy S7 Edge ya Rangi ya Coral Blue

Samsung imepanga kuongeza matoleo kwenye simu zake za samsung galaxy s7 kwa kuongeza rangi
Galaxy S7 Edge Galaxy S7 Edge

Hivi karibuni kampuni ya teknolojia ya Samsung imetangaza kuongeza idadi ya simu zake za Samsung Galaxy S7 kwa kuongeza rangi nyingine kwenye matoleo ya simu hizo. Samsung iliamua kuongeza rangi ya Coral Blue kwenye toleo jipya la simu ya Galaxy S7 Edge ambayo inategemewa kutoka hivi karibuni.

Simu hiyo mpya ya Samsung itanzaa kutoka kuanzia November 18 au November 22 mwaka huu kwa nchi ya marekani na baadae kusambaa kote duniani. Kampuni na Mtandao wa simu wa AT&T umetangaza kuwa ndio itakuwa ya kwanza kuwa na simu hiyo mpya ambayo inaonekana kupendwa sana na watumiaji wa simu hizo za Samsung Galaxy S7.

Simu hiyo mpya bado inayo sifa zake za awali za kioo cha inch 5.5 chenye kutumia teknolojia ya edge, processor ya Snapdragon 820 ikiwa na RAM ya 4GB pamoja na (storage) ukubwa wa memory ya ndani wa GB 32 na GB 64. Simu hiyo pia bado inatumia toleo la Android 6.0 Marshmallow lakini simu hiyo inategemewa kupata toleo jipya la Android 7.0 Nougat siku za karibuni.

Advertisement

Ili kujua ni lini simu hii mpya ya Galaxy S7 Edge itafika Tanzania endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use