Instagram Kutoa Taarifa Maalum Unapochukua Screenshot

Instagram kuanza kuonyesha taarifa maalum unapochukua screenshot ya private meseji au picha za mtu
Instagram Kutoa Taarifa Maalum Unapochukua Screenshot Instagram Kutoa Taarifa Maalum Unapochukua Screenshot

Hivi karibuni kumezuka gumzo ambapo imethibitishwa kuwa instagram sasa ita-anza kutuma meseji maalumu pale tu mtu atakapo chukua screenshot ya picha au meseji ambazo zipo kwenye private meseji.

Katika picha hapo chini ni moja kati ya meseji hiyo inavyoonyesha pale mtu atakapo chukua screenshot ya picha au meseji za mtu. Sehemu hiyo mpya ambayo haijajulikana kama imeshanza kuonekana kwa watu wote imechukuliwa kwa namna tofauti ikiwa wapo walio furahia na walio chukia ujio wa sehemu hiyo.

gallery-1480267726-screenshot

Advertisement

Instagram imeamua kufuata nyayo za mtandao wa snapchat ambayo nayo pia hutuma meseji maalum pale mtu atakapo chukua screenshot ya picha ama meseji za mtu pale ambapo haitakiwi kufanya hivyo.

Je nini maoni yako kuhusu sehemu hiyo mpya.? tuandikie hapo chini au pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use