Linapokuja swala zima la kutafuta movie au nyimbo fulani ukweli ni kwamba kuna tovuti nyingi sana za kusaidia katika hilo, lakini pale linapokuja swala zima la kutafuta movie na nyimbo mpya hapa ndipo kunapokua na mthiani mkubwa.
Hapo awali nilikua nikitumia karibia nusu saa au hata saa nzima kutafuta filamu au nyimbo fulani na tena naweza hata nisipate nachota hivyo kiukweli nilikua nikipata shida sana. Kama wewe bado unaendelea kuteseka kupata filamu na nyimbo mpya basi endelea kusoma makala hii.
Ukija kwenye swala la muziki ukweli ni kwamba tovuti nyingi za sasa hua ni lazima wamiliki wake wafanye kazi nzito ya kuweka nyimbo hizo kwenye tovuti hiyo hivyo pale mmiliki anapokua bize na mambo mengine basi unakuta wewe unakosa kupata nyimbo mpya ambazo nimpaka mimiliki wa tovuti apate muda wa kuziweka ndipo wewe huzipate.
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanasubiri hilo basi usiwe na wasi wasi kwani leo nimefanya ugunduzi ambao utaweza kukusaidia sana pale unapotafuta filamu na nyimbo yoyote ile mpya. Basi moja kwa moja Let’s Get to it….
YALIYOMO
Jinsi ya Kudownload Nyimbo Yoyote Mpya
Tofauti na tovuti nyingine tovuti hii ai-hifadhi nyimbo yoyote ile kwenye server zake bali inafanya kazi kama ilivyo Google au Search engine ya aina yoyote, tovuti hiyo inatafuta nyimbo hizi kutoka kwenye mtandao na kukuletea wewe ili uweza kudownload au kusikiliza vilevile tovuti hii inakusaidia kufanya vyote hapo hapo cha msingi ni kwamba unatakiwa kujua tu jina la nyimbo au msanii unae mtafuta.
Tovuti hii inayo nyimbo za wasanii wote iwe watanzania au hata wa nje ya tanzania cha msingi wewe ni kujua jina la msanii au jina la wimbo. ili kudownload nyimbo yoyote mpya bofya hapo chini kisha angalia video hapo chini kwa maelezo zaidi.
Jinsi ya Kudownload Filamu (Movies) Mpya
Kwa kuanza basi unachohitaji ni kuwa na bando pamoja na kuwa na programu ya IDM au Internet Download Manager, ninapendekeza programu hii kwa sababu programu hii inauwezo wa kuchukua (Automatic) file lolote lenye mfumo wa video au hata Audio hivyo na uhakika itakua ni rahisi kwako ukitumia programu hii kwa kua inavuta mafile hayo kutoka kwenye tovuti bila hata wewe kuteseka sana, kwa wale ambao wamesha wahi tumia programu hii basi lazima mtakua mnanielewa ninacho maanisha hapa.
Baada ya hapo hatua ya pili ni kubofya hicho kitufe hapo chini kisha utapelekwa kwenye tovuti ambapo utaruhisiwa kuangali filamu yoyote ile bure kabisa. Ili kudownload fuata maelekezo kwenye Video.
Bila shaka kwa kufuata maelezo hayo utakua umepata nyimbo ama filamu (Movie) uliyokua unaitafuta kwa muda mrefu.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.