Kampuni ya Snapchat Yabadilika na Kuwa Snap Inc.

Sasa inatengeneza bidhaa zaidi, yaja na bidhaa yake mpya ya Spectacles!
kampuni-ya-snapchat-yawa-snap-inc kampuni-ya-snapchat-yawa-snap-inc

Kampuni maarufu ya Snap Inc. ambayo hapo awali ilikua ikiitwa Snapchat sasa imeamua kujikita katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zaidi ya mtandao wake maarufu wa Snapchat, uamuzi wa kubadili jina hilo umekuja baada ya kampuni hiyo kuleta bidhaa yake mpya ya kwanza ambayo ni tofauti na mtandao huo.

Spectacles! ndio jina la bidhaa hiyo ambayo ni miwani mpya iliyounganishwa moja kwa moja na mtandao wa snapchat ili kukupa urahisi wa kukamata matukio muhimu kwa njia ya video na kisha kuyatuma moja kwa moja kwenye programu ya Snapchat. Hata hivyo katika post aliyopost mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa jina moja la Evan alisema kua imepita miaka mitano toka yeye na mmiliki mwenzake kwa jina moja la Bobby kugundua mtandao wa Picaboo ambao kwa sasa ndio Snapchat, katika safari hiyo wamefanikiwa kuwa na idea nyingi mbalimbali ambazo sasa zimezaa matunda hadi kufikia kampuni hiyo kuja na bidhaa hii mpya, Evan aliongeza kuwa watu wakae tayari kwani kampuni hiyo inategemea kuja na bidhaa nzuri zaidi zitakazo leta mabadiliko kwenye ulimwengu mzima wa teknolojia.

https://www.youtube.com/watch?v=XqkOFLBSJR8

Advertisement

Kampuni hiyo sasa inafanya promosheni ya bidhaa yake hiyo ambayo siku sio nyingi itaingia sokoni kwa jina hilo la Spectacles!. Hata hivyo miwani hizo zinategemewa kuingia sokoni zikiwa na rangi tatu za blue, nyekundu na nyeusi pamoja na kuunganishwa na moja kati ya kamera ndogo duniani zinazotumia wireless na bluetooth ili kukusaidia kuchukua matukio ya kumbukumbu zako moja kwa moja na kuyatuma kwenda kwenye mtandao wako wa snapchat.

Kujua zaidi kuhusu mtandao huo wa Snapchat pamoja na bidhaa yao mpya ya Spectacles!, endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use