in

Tovuti ya Kupakua Filamu na Muziki ya Kickass Torrent Yafungiwa

Tovuti Hiyo Yafungiwa na Serikali ya Marekani kwa Uvunjaji wa Haki Miliki

Kiongozi wa tovuti za kickass Torrent maarufu kwa jina la Artem Vaulin miaka 30 hivi karibuni ameshitakiwa na serikali ya marekani kwa kuendesha tovuti ya kickass torrent inayokiuka sheria za hati miliki, Artem Vaulin alikamatwa nchini poland baada ya mtego uliowekwa na FBI siku ya Jumatano ya tarehe 23 mwezi June Mwaka huu.

Kuondolewa kwa tovuti hiyo imekua ni pigo kubwa kwa wana Torrent kote duniani ambao hupenda kupakua vitu mbalimbali bila kulipia, hata hivyo blogu mbalimbali za maswala ya teknolojia nchini marekani zimeandika kuwa hivi karibuni kampuni za Sony Pictures, the Walt Disney Company (DIS), Warner Bros. Entertainment, na Universal Music zimekua zikiishinikiza serikali ya marekani kushulikia swala zima la haki milliki ya kazi mbalimbali zinazotengenezwa na kampuni hizo pamoja na wasanii wote wa marekani kwa ujumla.

Hata hivyo katika hatua za kumkamata kiongozi wa tovuti hizo serikali ya marekani iliomba serikali ya poland kumkamata na kumpeleka marekani kiongozi huyo ambapo alikua akishitakiwa kwa usambazaji wa kazi mbalimbali za wasanii bila kuzingatia haki miliki, Artem Vaulin alikua akishitakiwa kwa makosa mengine mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupoteza kazi za wasanii zenye thamani zaidi ya dollar za kimarekani $1 billion ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania TZS 2197000000000.00.

Je Kuwa na Subscriber Wengi Ndio Kupata Pesa Nyingi YouTube

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.