in

Programu 10 Bora za Habari Kwenye Vifaa Android

Soma habari kila siku kwa kuwa na programu hizi bora za habari Tanzania

Kama unatafuta programu bora za android kwaajili ya kukupa habari kwa hapa tanzania basi unasoma blog sahihi kwani hapa tunakurahisishia kwa kukusanyia programu 10 bora za habari kwa wale wanaotumia simu zenye programu za Android. kwa wale mnaotumia vifaa vya apple msijali programu zinakuja hivi karibuni na tuta kukusanyia hapahapa kwenye blog ya tanzania tech, oky basi twende tukazihesabu programu hizi bora za habari kwa wenye android programu.

KUMBUKA: List hii inaweza kubadilika wakati wowote kutokana na kuwa programu zinakuja mpya kila siku hivyo tutakua tuki-update list hii kila mara tutakapo gundua kuna programu mpya inayofanya vizuri imeingia. Pia List hii haijapagwa kufuatana na namba bali hizi zote ni programu bora za habari kwenye android.

Millard Ayo App

millard ayo
Price: Free

Kwa hapa tanzania kuna programu nyingi mbalimbli za habari lakini millard ayo app ni programu ambayo utakupa habari zote kubwa ziwe ni udaku, siasa. michezo au hata burudani programu hii ni changuo sahihi kwako.

Muungwana

Muungwana
Price: Free

Hii ni programu nyingine tena ya habari ambapo inakupa habari nyingi za mastar wa bongo magazeti pamoja na mambo mbalimbali ikiwemo maswala ya jamii pamoja na michezo.

Sasa Utaweza Kuwasha Muonekano wa Giza Kupitia Play Store

Kurasa | Tanzania News

Hii ni programu ya android inayokupa habari mbalimbali kutoka kwenye blog mbalimbali za tanzania, pia programu hii inakupa habari zote kuanzaia habari za siasa, michezo, utamaduni, mpira na mambo mengine mbalimbali.

Simu TV

SIMU.tv
Price: Free

Hii ni programu ambayo inakupa habari kwa kukusanyia na kukuonyesha live habari kutoka katika vituo vya televisheni mbalimbali vya tanzania, hivyo kama ilivyo jina lake hii ni programu nzuri ya kukuweka up to date kwa habari zote kutoka katika vituo vya video tanzania.

Clouds TV

Clouds TV
Price: Free

Hii ni nyingine inayokupa habari pamoja na breaking news zote kutoka tanzania na nje ya nchi kwa hivyo kama unataka kuwa na information na habari zote kwa siku nzima hii pia ni programu ya kupakua kwenye simu yako.

M-Paper

M-Paper
Price: Free+

Kama unatafuta kusoma magazeti ya kila siku hii ni programu nzuri sana ya kupakua kwenye simu yako kwani haina matangazo na ni bora sana pale unapokuja kwenye issue nzima ya magazeti.

App za Kukusaidia Kufanya Kazi Kwa Urahisi Ukiwa Nyumbani

Magazeti

Magazeti
Price: Free

Hii ni programu nyingine ya magazeti inayokuruhusu kusoma magazeti moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi, pakua app hii sasa.

Shaffih Dauda

Programu 10 Bora za Habari Kwenye Vifaa Android
The app was not found in the store. 🙁

Kama unatafuta habari zote za michezo hii ni progamu nzuri sana ya kuwa na inakupatia info zote za mambo ya mpira au michezo yote kwa ujumla programu hii ni bora sana.

Umbea Mtupu

Umbea Mtupu
Price: Free

Hii ni kwaajili ya wale mnaopenda habari za kunyapi nyapi, kwa habari zote za town kuhusu udaku na ubuyu wa town app hii ni kwaajili yako.

Tanzania Tech

Kama unataka kupata habari zote za teknolojia kutoka nje na ndani ya tanzania kwa kiswahili basi App hii ni bora sana kwako.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka,pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa.

 

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 3

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.