Mapema wiki hii, Xiaomi kupitia chapa yake ya Poco ilitangaza kuzindua mfululizo wa simu za Poco X7 tarehe 9 Januari. Ingawa hawakutaja idadi ya simu zitakazozinduliwa, sasa imethibitishwa rasmi kuwa kuna simu mbili: Poco X7 na Poco X7 Pro. Poco bado haijatoa maelezo kamili ya vipimo vya simu hizo, lakini imefichua kuwa Poco X7 Pro itatumia prosesa ya MediaTek Dimensity 8400 Ultra na kuwa na betri ya ukubwa wa 6,000 mAh.
Bei ya kuanzia ya Poco X7 Pro itakuwa chini ya INR 30,000 (takriban TZS 900,000), lakini haijabainishwa kama hii itakuwa bei ya uzinduzi au bei Halisi. Poco pia imeonyesha muundo wa Poco X7 na X7 Pro. Poco X7 ina paneli ya nyuma ya ngozi yenye kamera tatu, wakati Poco X7 Pro ina kamera mbili na muundo wa rangi mbili unaokumbusha toleo la Realme 10 Pro Coca-Cola Edition. Kamera kuu ya simu zote ina sensa ya 50MP yenye OIS.
Simu hizi zitauzwa nchini India kupitia Flipkart, ambayo imefichua kuwa X7 Pro itakuja na RAM ya LPDDR5X, hifadhi ya UFS 4.0, mfumo wa uendeshaji wa HyperOS 2, na uwezo wa kuchaji wa 90W.